Header Ads Widget

DART KUANZA KUTUMIA KADI JANJA, VIJANA KUTOKA IDARA YA TEHAMA WANOLEWA




Na fatma Ally, Matukio DaimaApp, Dar 


Wakala wa Mabasi yaendayo haraka (DART) leo wamefunga mafunzo kutoka kwa wataalamu wa idara ya Tehama  ambayo yamejikita katika matumizi ya kadi janja ambazo zinatumika kwa mfumo wa nauli.


Aidha, kupitia kadi hizo janja mteja hatalipa pesa keshi bali atalazimika kutipa kwenye mageti ambayo yamefungwa mfumo maalum wa kusoma kadi hizo ambazo zina ulinzi na usalama wa nywila atakazotumia mteja.


Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufunga mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Wakala wa Mabasi yaendayo haraka Dart,  Athumani Kihamia amesema kuwa mafunzo hayo yamelenga kutoa ujuzi kwa vijana mahiri ambao watayatumia kwa muda mrefu katika kutoa huduma zenye ubora.





 Amesema kuwa, Dart imetoa  mafunzo kwa vijana 10 ambayo yamedumu kwa siku tano yakiendeshwa chini ya usimamizi wa Mkyrugenzi wa tehama kutoka Dart na kampuni ya Advan ID kutoka nchini India yenye makao makuu yake nchini Singapoor.


Hata hivyo, amesema hadi sasa mageti zaidi ya 300 yameshafika huku ujenzi wake ukikamilika kwa asilimia 67 ambapo yamegharim zaidi ya bill 11 lengo ikiwa ni kusaidia kudhibiti mapato kwa watumishi wasio waaminifu,.


"Kadi janja ni kadi zinazotumika katika mfumo wa nauli lengo la Dart ni kuwa maeneo mengi na kuwa na timu kubwa ya vijana mahiri ambao tutakaa nao kwa miaka 10 ili iwe rahisi kupeana ujuzi na vijana wengine wapya watakao ajiriwa, tunataka kuboresha mifumo yetu ili tutoe huduma zenye ubora"amesema Kihamia.


Hata hivyo, amesema kuwa siku chache zijazo baada ya mwezi wa 6 wataanza kutumia mageti hayo ambapo wameshaingiza mageti janja kutoka nje zaidi ya 300, yatatumika katika mfumo wa nauli yataepusha katika uvujaji wa nauli, mapato na watumishi wasio waaminifu, pamoja na kuokoa muda.


Naye Mkurugenzi wa Teknolojia habari na mawasiliano Tehama Dart Ng'wanashigi Gagaga amesema baada ya Mafunzo hayo lengo ni kujenga uwezo wa timu ya   wanaoshughulikia mfumo wa nauli katika mageti yatakayotumia mfumo wa kadi hivyo  mpaka sasa kituo cha Korogwe kimeshakamilika na vingine vinaendele na matengenezo.


"Ubora wa Mageti haya janja yatakayofungwa mfumo maalumu  na kuanza kutumika abiria atakapofika na kadi yake itamwonyesha kiasi cha fedha kama hakitoshelezi akaongeze hivyo hakutakiwa na matumizi yeyote ya karatasi tuko kidigital zaidi " amesema Mkurugenzi Tehama .


Awali mafunzo hayo yaliwahi kutolewa mwaka 2000  lakini kutokana na kuhamishwa hamishwa kwa watendaji wamelazimika kutolewa tena mwaka 2024, huku wakiahidi kuendelea kutoa mafunzo hayo tena.


Katika hatua nyengine, amewaonya madereva wanaoendesha magari ya Serikali, boda boda na magari binafsi kuacha kutumia njia ya mwendokasi bila kibali maalum kwani kufanya hivyo ni kuvunja sheria na kusababisha ajali zisizo za lazima.


Naye Muhitimu wa Mafunzo hayo Jackson Kazaura ameshukuru kupata mafunzo hayo hivyo ameahidi ujuzi huo anakwenda kuutumia na kufundisha wengine .


Kwa upande wake,Mwezeshaji wa mafunzo hayo Kutoka Kampuni ya Advan IDe, Duncan  Chege amesema wametoa mafunzo kwa ubora mkubwa hivyo wanaamini mafunzo waliyoyatoa kwa wahitimu hayo yatakwenda kuzaa matunda mazuri katika kuboresha ubora wa huduma watakazozitoa kwa wateja kupitia kadi janja.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI