Header Ads Widget

ASASI ZA KIRAIA 15 KUFIKISHA MALALAMIKO YAO YA KUKWAMISHA KAZI ZAO BUNGENI NA SERIKALI




Na Ashton Balaigwa,MOROGORO

MASHIRIKA  15 yasiyo ya Kiserikali ya Asasi mbalimbali kutoka Tanzania Bara na Visiwani(ZANZIBAR),yanakusudia kufikisha mapendekezo yao  ikiwemo ya Kisheria,Kisera na Kiutendaji kwenye vyombo vya Maamuzi  likiwemo Bunge na Serikali ili kuyawezesha  kufanya kazi katika Mazingira mazuri na kuleta maendeleo nchini.

Hatua  ya kupeleka mapendekezo hayo kwenye vyombo vya maamuzi ni baada ya kukutana kwa lengo la kujadili na kufanya uchechemuzi wa changamoto zinazo tokea katika mashirika hayo ikiwemo uboreshaji wa sheria na taratibu za ulipaji kodi na kujikuta yakifanya kazi katika mazingira magumu.

Akizungumza Mjini Morogoro na Kaimu Mkurugenzi wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) , Wakili MarkPhason Mshana alisema wamekutana na wadau wa Asasi hizo ili kupitia maoni yaliyokusanywa kutoka kwenye asasi hizo nchini nzima.

Wakili Mshana alisema kupitia mradi wa URAIA WETU  unaofadhiliwa na Umoja wa Nchi za Ulaya(EU) unaotekeleza na Asasi ya Kiraia ya Foundation For Civil Society ( FCS) unaangalia kuweka mazingira mazuri kwa asasi hizo kufanya shughuli zao.

Alifafanua Mazingira yanayoangaliwa yapo katika maeneo matatu ambayo ni Kisera,Kisheria na Kiutendaji na kikubwa wanachotaka kupeleka kwenye vyombo vya maamuzi ni kutokana na Asasi za Kiraia kama muhimili wa sita wa shughuli za nchi waweze kuwa na nafasi nzuri za kufanya kazi kazi bila ya kuwa na mikwamo.

), “ Lengo letu kama wadau wa shughuli za maendeleo ya nchi Asasi za Kiraia tunataka ziweze kufanya kazi bila mikwamo ya  Kisera,Sheria na Kiutendaji hivyo tunakutana na wadau mbalimbali kutoka katika kila mkoa na tumepata maoni mengi hivyo tumeamua kukaa pamoja ili kukubaliana nini changamoto tuanze kufanya uchechemuzi” alisema Wakili Mshana.

Alisema malalamiko mengi ambayo yanatoka kwa wadau hao ni kuhusu kuwepo kwa sheria nyingi za  Asasi za kiraia kuangalia sekta hiyo ambazo kuna wakati zinawachanganya ni sheria ipi wanatakiwa kuifuata .

Alisema kupitia mkutano huo wanaangalia kuwa na sheria moja ambayo wataifuata Asasi zote ili kila moja aweze kujua anaifuata sheria hiyo na kwa wakati mmoja .

Malalamiko mingine ni pamoja na Asasi hizo pamoja na kufanya kazi za kiraia ambazo zilipaswa kufanya na Serikali lakini bado zimekuwa zikitozwa kodi mbalimbali jambo ambalo halileti tija.

“ Zipo kodi kama za wafanyakazi hizo hazileti changamoto lakini changamoto ipo kwa  zile shughuli ambazo Asasi wanazifanya lakini wanatozwa kodi kwa mfano wanapoagiza vifaa kwaajili ya shughuli fulani  unakuta zinatozwa kodi wakati asasi  mara nyingi zinategemea ufadhili na Wafadhili hawaweki kipengele cha tozo kwakuwa wanaamini asasi hizo zinafanya kazi kwa niaba ya serikali” alisema Wakili Mshana.  Naye  Jehn Magigita ambaye  Mkurugenzi Mtendaji wa  Asasi ya Quality For Growth alisema Mradi wa URAIA WETU unalenga kuangalia usawa wa kijinsia na sheria ambazo zitasaidia kutengeneza mazingira wezeshi kwa ajiri ya makundi maalumu.

Nae Mratibu wa Mtandao wa Utetezi wa Haki za Binadamu Zanzibar,(THDRC) Suleiman Baitani alisema katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku suala kubwa linaloibuka katika sekta ya Asasi hizo za Kiraia ni swala la kodi ambalo linahusisha pande zote mbili za Muungano kwakuwa linatumia Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA).

Alisema jambo kubwa linaloibuliwa na Asasi hizo ni kufananishwa na wafanyabiashara kama watu wanaokusanya kodi na mwisho wa siku inawapa changamoto kubwa kwenye kulipa kodi wakati inatoa huduma kwa niaba ya serikali.

“Utakutaka Asasi ya kiraia haijapata mradi muda mrefu halafu inajikuta ina malimbikizo ya madeni yanayofikia milioni 300 mpaka 400 sasa sisi kuna huduma nyingine tunazitoa sio za kukusanya kodi  bali tunasaidia wananchi” alisema Baitani.
Mwisho
Maelezo ya Picha
Kaimu Mkurugenzi wa Chama Cha Mawakili Tanganyika(TLS) Wakili Markphason Mshana,kulia akizungumza na waandishi wa Habari mjini Morogoro kuhusu Asasi hizo kifikisha malalamiko Yao kwenye vyombo vya maamuzi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI