Header Ads Widget

WAZIRI MKUU AWAAGIZA WAKUU WA MIKOA WOTE

 



Na Hamida Ramadhan Matukio Daima app Dodoma

WAZIRI Mkuu  Kassim Majaliwa Kassim amewataka wakuu wa Mikoa kote nchini Kutoa ushirikiano Kwa kikosi kizima zitakachoshiriki Katika ukusanyaji wa maoni ya Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2050.

Hayo yameelezwa leo Leo jijini Dodoma,wakati akifungua semina ya wakuu wa mikoa kuelekea zoezi la ukusanyaji maoni ambapo ameeleza kwamba ili kufanikisha zoezi hili lazima kuzingatia maadili ya kitanzania na kudumisha Umoja na ushirikiano. 

Pia amewataka wakuu hao wafanye ufuatiliaji wa zoezi hilo katika maeneo yao ya kiutawala na kutoa taarifa mara kwa mara sambamba na kuandaa ripoti za kila wiki ili iwe rahisi kufahamu mwenendo wa zoezi hilo.

Amesema ili zoezi hilo la kutoa maoni ya Dira mpya liende vizuri hawana budi kushirikiana bega kwa bega na viongozi wa dini.

"Mmekuwa wakati wote mkishirikiana na Serikali kutoa hamasa kuhusu masuala muhimu ya Kitaifa. Nitoe rai kwenu mshiriki kikamilifu katika utoaji maoni lakini pia kutoa hamasa kwa waumini wenu,” amesema Waziri Mkuu

Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mipango na Uwekezaji), Prof. Kitila Mkumbo amesema hadi sasa wananchi 623,614 tayari wametoa maoni kuhusu Dira ya Taifa kupitia kwenye mtandao (portal).


Amesema kuwa kati ya waliotoa maoni hayo, asilimia 70 ni wanaume huku idadi kubwa ya walijitokeza ikiwa ni vijana wenye umri wa kati ya miaka 15-35.



Awali, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Dkt. Tausi Kida, alieleza hatua mbalimbali kuhusu mchakato wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, tangu ulipoanza 2021 hadi Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alipozindua mchakato wa ukusanyaji wa maoni Desemba 9, 2023 na hatua zilizofanyika hadi kufikia semina hiyo kwa Wakuu wa Mikoa.

Naye Naibu Waziri TAMISEMI Dkt, Festo Dugange ameahidi kutekelezwa kwa dira hiyo kwa ufanisi .

Semina hiyo ya wakuu wa mikoa inakuja wakati taifa la Tanzania linajiandaa na zoezi la ukusanyaji wa maoni ya wananchi na wadau katika kuandaa dira ya taifa ya maendeleo 2050.


Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS