Header Ads Widget

WAKUU WA WILAYA WATATU MKOANI KILIMANJARO WAKABIDHIWA MAGARI..



Na WILLIUM PAUL, MOSHI. 




MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu amekabidhi  magari matatu kwa ajili ya wakuu wa wilaya za Rombo, Mwanga na Same ili kuongeza ufanisi wa utendaji  na kuleta maendeleo  ya mkoa yenye thamani ya zaidi ya milioni 200.


Akizungumza  katika hafla  fupi ya makabidhiano  hayo nje ya viwanja wa ofisi za mkuu wa mkoa, Babu alisema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameanza kutekeleza maombi mbalimbali ya mkoa wa Kilimanjaro ya kuwapatia Wakuu wa wilaya vitendea kazi.




Babu alisema kuwa, Wabunge wamekuwa wakilalamika Bungeni kuhusiana na wakuu wa wilaya kukosa magari ambapo mkoa ulipanga kuhakikisha bajeti ya mwaka wa fedha 2023/24 mpaka ifikapo mwezi Juni mwaka huu wawe wameshanunua magari matatu ya wakuu wa wilaya.


"Haya magari matatu tulipanga kuhakikisha tunayanunua mwaka huu wa fedha lakini pia tumejiwekea malengo kwa mwaka wa fedha 2024/25 tunanunua magari mengine matatu ya wakuu wa wilaya waliobakia" alisema Babu.



Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa, magari hayo yatatumika kwa ajili ya shughuli za kiserikali na kuwataka kwenda kuyatunza magari hayo kwani yamenunuliwa kwa gharama kubwa.


Aliwataka kuhakikisha kuwa wakati wa sevisi yanakwenda sevisi na pia madereva kukagua gari kabla ya kuliwasha na kuondokana.



Aidha Babu amewataka Wakuu wa wilaya kuwaachia Madereva wafanye kazi zao kwani ndio waliyosomea kuendesha gari na kuachana na kumwambia kuvunja sheria ili kuwahi kule unapoenda ili kuepuka ajali zisizo na ulazima.


Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya Rombo, Raymond Mangwala alimshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwajali wasaidizi wake na kuwapa vitendea kazi na kuahidi kutumia gari hilo kufanya kazi iliyokusudiwa ikiwemo kuhakikisha miradi inaenda kukamilika.



"Kitendea kazi hiki ambacho nimekabidhiwa namuahidi Rais nitaenda kukitumia kwa kazi zilizokusudiwa za kuwatumikia wananchi wa wilaya ya Rombo ili malengo yake yaweze kutimia" alisema Mangwala.



Aidha aliwataka viongozi  wote wanaotumia magari ya umma kuheshimu sheria taratibu na kanuni za uendeshaji wa magari  unaotolewa na madereva ili kuepusha ajali zinazoweza kuepukika.



"Hile ni ofsi ya dereva, hakikisha unaiheshimu kila mara na kupokea ushauri wao, tuwasikilize mara kwa mara ili kuleta matokeo chanya, 



Naye  mkuu wa wilaya ya Same,  Kasilda  Mgeni  alisema kupatikana kwa vitendea kazi kutachangia  kuwafikia  wananchi na kutatua kero zao .



Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS