Header Ads Widget

VIJANA 200 WAHITAJIKA KUCHANGAMKIA FURSA ZA KILIMO NA UJASIRIAMALI NJOMBE

 Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE

Wakati serikali ya Wilaya ya Njombe ikifanikiwa kuunda vikundi 70 vya vijana kwa ajili ya kuwawezesha kupitia fursa mbalimbali za kilimo na Ujasiriamali duru zimeeleza kuhitajika kwa vijana wengine 200 wanaotakiwa kuchangamkia fursa hizo.

Miongoni mwa fursa zinazotajwa ni pamoja na kilimo cha Viazi mviringo, Parachichi, Mbogamboga na hata shughuli za viwanda vidogovidogo ambapo Mkuu wa wilaya ya Njombe Mhe. Kissa Kasongwa anasema wadau mbalimbali wakiwemo wakala wa hifadhi ya Misitu Tanzania TFS  wameahidi kufadhili baadhi ya fursa hasa za misitu.

Kituo hiki kimezungumza na baadhi ya Vijana akiwemo Marko Mhagama na Zuhura Benela ambao wamesema wanatamani kujishughulisha na kilimo kwani wamegundua kilimo kinalipa.

Vijana wengine akiwemo Nicko Mgaya wanalia na changamoto zinazotatizo sekta ya Kilimo ikiwemo gharama kubwa ya mbolea,mimea kushambuliwa na wadudu waharibifu na kuomba serikali kuwasaidia kukabiliana nazo.

Kwa upande wao baadhi ya wazazi mkoani Njombe akiwemo Ruben Mtitu wanakiri kuwapo kwa changamoto ya Ajira kwa vijana wao na kwamba fursa hiyo iwe mwarobaini kwa watoto wao.

Mei 6 mwaka huu vijana hao watakutanishwa na kuingia kambini kwa siku tatu ili kuratibu shughuli watakazoanza kuzitekeleza.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI