Header Ads Widget

USIKU WA MUUNGANO WAFANA SONGWE, RC CHONGOLO AWANG'ATA SIKIO WANANCHI JUU YA KUULINDA MUUNGANO.

Na Moses Ng'wat, Mbozi.

VIONGOZI mbalimbali Mkoa wa Songwe wakiongozwa na MKuu wa Mkoa wa huo, Daniel Chongolo na Katibu Tawala (RAS) Happiness Seneda wameshiriki usiku wa muungano.


Tukio la usiku wa Muungano limeandaliwa na ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mbozi na kufanyika leo Aprili 25, 2024 katika viwanja vya CCM Vwawa,Wilayani Mbozi, ambapo idadi kubwa wamejitokeza kushiriki.



Katika tukio hilo, shughuli mbalimbali zimefanyika, ambapo viongozi hao wa Mkoa, watendaji na wananchi wa kawaida wamepata fursa ya kusikiliza na kufuatilia hotuba ya Rais Samia Suluhu Hassan kupitia Runinga kubwa zilizowekwa uwanjani hapo.


Mbali na Hotuba ya Rais, pia shughuli hiyo imeambatana na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii wa Mkoa Songwe, ikiwemo Bendi ya muziki ya Itaka inayomilikiwa na Jeshi la Wananchi (JWTZ) kikosi cha Itaka, Wilayani Mbozi.


Akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa kwa ajili ya kusalimia wananchi katika tukio hilo, Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe, Seneda ametumia fursa hiyo, kuupongeza uongozi wa Wilaya ya Mbozi kwa maandalizi makubwa ya tukio hilo lililofana.




Kwa upande wake, Chongolo, akitoa salamu kwa wananchi, 

alisema hotuba iliyotolewa na Rais ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 60 ya muungano.


Hata hivyo, amewataka wananchi wa Mkoa wa Songwe kuendelea kuuenzi muungano hasa kwa  kutafakari ujumbe uliotolewa na Rais kupitia hotuba hiyo.


"Kwa pamoja tumrsikiliza hotuba ya Rais kwa makini...mimi sitaki kuongezea kitu chochote kikubwa kila mmoja wetu achukue ujumbe uliotolewa na  kufanyia kazi ili tuendelee kuudumisha muungano wetu" alisema Chongolo .


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS