Header Ads Widget

TRA KAGERA YAHIMIZA WAFANYABIASHARA KUTOFANYA BIASHARA ZA MAGENDO.


.

Na Shemsa Mussa,Kagera 

 Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Mkoa  Kagera imewataka na kuwawashauri wafanyabiashara  wa mkoa huo kutofanya biashara za magendo ili kuepuka athari za kiuchumi ikiwemo   kuikosesha  kodi Serikali hali inayofanya  kushindwa kutoa huduma stahiki kwa wananchi.

Meneja wa mamlaka hiyo Castro John ameeleza hayo leo wakati akiongea na waandishi wa habari  ofisini kwake ambapo ,lengo ilikuwa ni kuhamasisha ulipaji kodi kwa ihari na kuonyesha mafanikio ya ukusanyaji kodi kwa kipindi cha Januari hadi Machi mwaka huu ambapo walilenga kukusanya shilingi Bilioni 28.4 na wamekusanya bil.30.2

“Tukikosa kodi Serikali haiwezi kutekeleza mairadi ya maendeleo mfano kama mnavyoona sasa hivi kuna mvua nyingi miundombinu kama madaraja yanachukuliwa na maji na Serikali inapaswa kurejesha katika hari nzuri kwa kujenga upya au kukarabati kama hatuna fedha hayo yote hayawezekani,viwanda  vya ndani kushindwa kuzalisha kutokana na bidhaa kuingia olela kutoka  nje pia inaleta athari kwa watu maana kama bidhaa imeingia hajadhibitishwa jamii ikatumia inaweza kudhulika ikiwemo vifo”amesema John

Ametaja athari nyigine ambazo zinatokana na magendo mipakani ni pamoja na uharibifu wa mazingira kwasabu mifuko ya plasiki ikiingia nchini kiholela inachangian kwa asilimia kubwa uharibifu wa mazingira,bei za bidhaa kupanda na wakati mwingine kusababisha vifo kwasababu wakati wa ukamataji watu wanakimbizana maana hakuna mtu anayekubali kukamatwa kirahisi.


Alisema mamlaka hiyo ipo kwa ajili ya kutoa huduma bora hivyo wale wanaofanya magendo waache mara moja kwasababu vyombo vya ulizni na usalama vipo kazini na wao wanafanya misako ya kila kona na kila sehemu za mipaka yetu hivyo,wanaojihusisha na magendo watawaona na kuwabaini kisha kuwachukulia hatua za kisheria.

Aidha John amewashauri wamiliki wa vyombo vya moto kuhakikisha wanapouziana vyombo hivyo kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine waende Tra watapata maelekezo ili waweze kubadilisha umiliki na kuepukana na adha na shida hususani za kiusalama ambazo zinaweza kujitokeza wakati chombo hicho kikikutwa kinatumika sehemu isiyostahili.

Ametoa ufafanuzi kuhusu madhara yatokanayo na kutobadilisha umiliki wa vyombo hivyo ambapo alitoa mfano unakuta pikipiki uliyouza miaka mitano iliyopita bila kubadilisha umiliki ikapatikana kwenye tukio la wizi au mauaji lakini bado jina lako linasomeka hivyo lazima ukamatwe wewe hivyo tujiepesha na madhara hayo.

Meneja huyo amesema kupitia mabadiliko ya sheria ya mwezi Julai 2023 ilielekeza wafanyabiashara wamiliki wa pikipiki (bodaboda) wote wanatakiwa kulipa kodi ambayo ni shilingi 65,000 kwa mwaka ambapo inalipwa kwa awamu nne huku, akiwataka bodaboda kutambua kuwa kutokulipa kodi ni kuvunja sheria na kama mtu hajaelewa kuhusu ulipaji kodi afike katika ofisi za TRa kagera ili apate elimu zaidi.

Wakati huo huo Afisa elimu kwa Umma wa mamla hiyo Rwekaza Rwegoshora alisema Serikali inategemea kodi  ambapo asilimia 70 ya mapato ya Serikali yanatokana na kodi hivyo hicho ndicho chanzo kikuu cha mapato ya nchi .

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS