Header Ads Widget

SHEKHE ABRI ATAKA BUSARA KUDAI KATIBA MPYA

 



NA MATUKIO DAIMA APP,IRINGA  

SHEIKH wa Waislam mkoa wa Iringa   Said Abri (pichani )amesema watanzania wanatakiwa kuendelea kudai katiba mpya kwa amani pasipo vurugu .



Akitoa salamu za Eid Leo mara baada ya Ibada ya Eid iliyofanyika uwanja wa Samora mjini Iringa,Sheikh Abri alisema tayari Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ameonesha nia ya kutaka katiba mpya na mara kadhaa amekuwa akisisitiza hilo.


Hivyo ni nafasi nzuri kwa Watanzania kuwa na subira wakati mchakato wa kupata katiba mpya ukiendelea .

"Suala la katiba mpya ni hitaji ya watanzania wote sio kikundi Cha watu ama mtu mmoja Pekee hivyo itakuwa si busara kwa kikundi ama mtu kufanya uchochezi ama vurugu wakati wa kuhitaji katiba mpya "

Kuhusu Uchaguzi wa serikali za mitaa unaotaraji kufanyika mwaka huu na Uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka Sheikh Abri alitaka watu wote wenye sifa ya kugombea kujitokeza na Siku ya Uchaguzi wenye sifa ya kupiga kura kushiriki kuchagua viongozi .

Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwada alisema salamu za Sheikh Abri zimejaa hekima zaidi.


Huku akishauri watanzania wenye sifa kujitokeza kwa wingi, kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa ambao unatarajiwa kufanyika mwaka huu pamoja na uchaguzi mkuu utakao fanyika hapo mwakani.




Katika hatua nyingine meya Ngwada, alikemea matukio ya ukatili ambayo yanaonekana kushamiri mkoa wa Iringa na kuwataka wananchi kuwa na tabia ya kutoa taarifa pindi wanapoona uwepo wa viashiria vya matendo ya ukatili ili kuweza kudhibiti matukio hayo, huku akiwakumbusha wazazi na walezi kuzingatia lishe bora kwa watoto wao kwa kwa kuhakikisha kila mlo unakuwa na makundi yote ya vyakula ili kupunguza udumavu na utapiamlo kwa watoto waliochini ya umri wa miaka 5.


 Kamishna wa chama cha ADC nyanda za juu kusini,  Daud Masasi aliwataka waislamu kuendelea kutenda mema ambayo walikuwa wakiyafanya kipindi cha mwezi wa Ramadhani kwa huko ndiko kumcha mungu na kusimimia nguzo za Imani.





Diwani wa kata ya Kwakilosa Hamid Mbata kushoto akimpiga picha mstahiki meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwada na waunini wa dini ya kiislam kwenye viwanja vya Samora baada ya Ibada ya Eid

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI