Header Ads Widget

MIONGONI MWA HABARI TULIZONAZO LEO 4/42024 KATIKA HOT NEWS NI

 


Rais Samia Suluhu Hassan ametaja sababu za kumteua Paul Makonda kuwa mkuu wa mkoa wa Arusha, huku akielezea anachokitegemea katika utendaji wake ndani ya mkoa huo.

 


 

Wakili wa kujitegemea Emmanuel Chengula amesema Sakata la Wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kama wamachinga manispaa ya Iringa limetokana na kuyumba kwa misingi ya utawala bora jambo ambalo limepelekea wafanyabiashara hao kupigwa, kuumizwa na kumwagiwa bidhaa zao na migambo, jambo ambalo linahatarisha usalama wa wafanyabiashara hao.

 


 

Mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Ibrahim Ramadhan  (44) mkazi wa kata ya Mwembesongo, manispaa ya Morogoro, amenusurika kifo baada ya kuangikiwa na ukuta wa jengo la ghorofa lililokuwa likijengwa katika mtaa wa Sugume, mkoani Morogoro.

 

 


 

 

Wananchi wa Kijiji cha Kambai kilichopo kata ya Kwezitu wilaya ya Muheza mkoani Tanga, wamechoma gari aina ya suzuki la afisa kilimo wa kata jirani ya Tongwe, pamoja na kumjeruhi afisa huyo, wakimtuhumu kushindwa kusimamia maslahi ya wananchi na kupelekea wawekezeji kupewa eneo la zaidi ya ekari 500 bila kufanyika kwa tathimini ya kina wala wananchi kushirikishwa.

 

 



Mkurugenzi wa shule za Sun Academ zilizopo manispaa ya Iringa Nguvu Adward Chengula ameita jamii kuwa na mikakati bora itakayo wawezesha kuondokana na umaskini ambao unaonekana bado unawakabili watanzania wengi.

 

 



 

Mahakama ya wilaya ya Mtwara imemhukumu kifungo cha Maisha jela, Asha Ismail Chanchoni (47) kwa kosa la shambulio la aibu baada ya kujihusisha kimapenzi na mvulana mwenye umri wa miaka 15.

 


 BOFYA LINK HII KUTAZAMA TAARIFA YA HABARI

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI