Header Ads Widget

WAJUMBE 1661 WA UWT KIBITI WAPIGA KURA ZA MAONI KUPATA MADIWANI VITI MAALUM KIBITI

 

NA MATUKIO DAIMA MEDIA KIBITI 

Mwenyekiti wa UWT wilayani Kibiti Tatu Mkumba ameongoza mkutano Mkuu wa jumuiya hiyo na kuongoza upigaji wa kura za maoni za kupata Madiwani wa viti maalum kwa tiketi ya CCM wa Jimbo la Kibiti mkoani Pwani ambapo Wajumbe 1661 wamepiga kura.


Akifungua mkutano huo Mkuu Tatu amewataka Wajumbe wa mkutano huo wa wilaya ya Kibiti Kufanya uchaguzi wa haki wenye lengo la kupata wagombea wazuri watakaoweza kuwafanyia maendeleo wanawake wa Wilaya ya Kibiti ambao umeratibiwa na Katibu wa UWT Kibiti Rabia Selemani.

 matokeo ya kura hizo za maoni Msimamizi wa Uchaguzi wa kura za maoni Zainabu Mketo katika viwanja vya CCM wilaya ya Kibiti amesema wagombea wa udiwani Viti maalum walikuwa 19 katika Tarafa tatu.

Amesema Tarafa ya Mbwela Swaumu Mwangi aongoza kwa kupata kura 923 kati ya kura 1661 akifuatiwa na Mwajuma Dagwa aliyepata kura 906 na watatu ni Ashura Ngonwe aliyapata kura 684.

Tarafa ya Kikale ameongoza Mwashabani Mlawa kwa kura 1265 akifuatiwa na Amina Mapande aliyepata 351.

Wakati Tarafa ya Kibiti aliyeongoza ni Latifa Augustino aliyapata kura 1338 akifuatiwa na Mwamtimu Hamza aliyepata kura 962 na nafasi ya tatu alipata kura 874 Salha Mjanja


.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI