Header Ads Widget

CHATANDA AONYA SIASA KWENYE KAMBI ZA WAATHIRIKA WA MAFURIKO RUFIJI








Na scolastica Msewa, Rufiji

Mwenyekiti wa UWT taifa Mary Pius Chatanda (MCC) ameonya jamii kuacha kutumia siasa kwenye kambi zilizotengwa na serikali  kwa ajili ya  waathirika wa mafuriko na badala yake wafike kwenye kambi ihzo kwa kuwafariji na kupatia msaada  watu  walioathirika wa mafuriko ya mto Rufiji.


Akizungumza baada ya kukabidhi msaada huo, mwenyekiti Chatanda amesema jumuiya ya UWT inatoa salamu za pole kwa wahanga wa mafuriko hayo, serikali na Watanzania kwa ujumla na kwamba imepokea kwa huzuni kubwa taarifa za athari zilizotokana na mafuriko hayo.


Alisema waachane na watu wanaokuja kutengeneza siasa huku, msiwasikilize wakianza kuongea muwaulize wamewaletea nini na misaada ya kutaka kuhutubia ikataeni ya kazii gani?


"Unawahutubia wenzako wakati wanamatatizo wanafikiria ni namna gani wataishi watoto wao hawaendi shule, nguo zimekwenda, chakula hakuna wewe unakuja kuhutubia kitu gani unaeleza kitu gani.


"Achaneni na watu wanaokuja kupiga siasa ambao hawaji kuwasaidia kwa misaada wanaokuja kuzungumza Siasa huku sio wakati wa Siasa sasa hivi ni wakati wa kuwasaidia wananchi wetu ambao wamepata changamoto hizo za maji"


"Nawaambieni kina mama wa Kibiti msikubaliane na watu wanaokuja kuwachonganisha huku wanaotaka kuichonganisha serikali na Wananchi, serikali inawapenda na ndio maana inawakimbilia nimekuja kuwaambieni Mimi mwanamke mwenzenu"


"Kama Serikali ilngekuwa haiwapendi Serikali isingechukua tafadhali na kutoa misaada iliyotoa achaneni na hao wanaokuja kuwapambanisha na serikali Rais wetu ni mtu mzuri" alisema Mama Chatanda.


Alisema "poleni sana kwa changamoto hizi na fikiri tuendelee kuomba Mwenyezi mungu aendelee kuwapa afya njema na kutuepusha na haya mambo ambayo yameendelea kutokea katika nchini yetu maana hayapo hapa tu kwa maana ya Kibiti na Rufiji tu bali haya mambo tukiangalia vyombo vya Habari yapo mikoa mingi" 


"Lakini pia jana nilikuwa naangalia kwenye vyombo vya Habari nimeona nje kule nchi ya Oman ambapo mafuriko ya huko hapa kuna nafuu kidogo yaani huko nchi za nje nako yapo, safari hii Mwenyezi mungu nadhani anatuonyesha jambo"


"Tumrudie Mwenyezi mungu tuwe tunasali ndugu zangu tuombe haya matukio yaweze kutuepuka ingawa tunajua watu wa Rufiji na Kibiti mnasema haya mambo mmeyazoea, huwezi kuzoea changamoto kama hizi tuombe Mungu, changamoto hizi hazizoeleki"


"Tuendelee kuwashawishi Wanawake wenzetu na wanaume waliko kwenye maeneo hatarishi maana serikali imeweka mipango mizuri sana kwa ajili yenu endeleeni kuwaelimisha Wanawake wenzenu na akinababa watoke kwenye yale maeneo hatarishi waje kwenye nchi kavu huku"


"Serikali imesema itawahudumia, Dkt Samia Suluhu Hassan amesema yeye atawaagiza watu wake Viongozi wa mkoa, Mawaziri kwamba hakikisheni wananchi wangu wanapata huduma zote na ndio maana hata yeye binafsi akaweza kuleta msaada huku"


"Tukiacha misaada ya serikali lakini ameleta msaada binafsi tani 300, Sasa kama kaleta tani hizo 300 si anawapenda? Mnataka afanyeje mwanamke wa Watu huyu basi tuendelee kuwashauri na kuwashawishi Wanawake wenzetu waliobaki kwenye maeneo hatarishi kule ili waweze kurejea huku kwenye maeneo makavu."


Aidha Mwenyekiti huyo wa UWT taifa alikabidhi misaada mbalimbali ya vifaa na mahitaji ya akinamama na familia zao yenye thamani ya zaidi ya shillingi milioni 76 na kugawa katika wilaya ya Rufiji na Kibiti.


Mama Chatanda amemkabidhi vifaa mbalimbali  ikiwemo mashuka 470, vyandarua 400 vyenye mabelo matano, vijora 500, unga wa sembe viroba 76, maharagwe kg 100, sukari kg 150, nguo mchanganyoko na ndogo kubwa za plastic 380.


Vifaa vingine vilivyotolewa ni mabeseni 400, sahani 442, vikombe 492,magodoro 47, nguzo za watoto belo 1, nguo za watoto wa kike belo 1, nguo mchanganyoko begi 3, mabegi ya shule 35, pampas pisi 10viatu mchanganyoko kiroba 1 na tambi mifuko 10.


Licha ya msaada huo pia wamekabidhi sabuni za mche boksi 10, sabuni za unga viroba 2, masufuria makubwa 5, MADAFTARI 500, mafuta ya kupikia ndogo 3, mafuta ya kupikia korie boksi 5, unga wa ngano kg 25 viroba 3, blanket belo 3 na mikeka 3.


Misaada mingine aliyopokea ni maharagwe kg 100, mchele kg 100, unga kg 500 mafuta ya kupikia lita 100 na sukari kg 100 kutoka Kampuni CRCEB.


Awali Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Kanali Joseph Kolombo alipokea magodoro 300, mafuta ya kupikia kg 5 lita 250, sukari ujazo wa kg 2 kg 250,  unga wenye ujazo wa kg 250,mchele wenye ujazo wa kg 5 kg 250 kutoka Kampuni ya Superdoll.

Awali akitoka taarifa ya hali ilivyo kwasasa katika wilaya hizo kwa Uongozi wa UWT taifa Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge alisema kutokana na kuharibika kwa miundombinu ya Barabara zoezi la usambazaji wa chakula hasa Kibiti linakuwa gumu hivyo wameomba.msaada wa magari ya jeshi la kujenga taifa wasaidie kufikisha chakula hicho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS