Header Ads Widget

KWANINI WANYAMA WENGINE HUFADHAIKA WAKATI WA KUPATWA KWA JUA?

Wanadamu hustaajabishwa na kupatwa kwa jua, lakini wanyama wengine huhisije mchana unapogeuka kuwa usiku kwa muda mfupi?

Katika matukio maalum sana, wakati hali inapokuwa sawa tu, mwezi huzuia jua na anga linakuwa jeusi.Ingawa kupatwa kwa jua kwa jumla hudumu kwa muda mfupi tu, kunaweza kuwa na athari kubwa kwa watu, kusababisha hisia za mshangao.

Lakini ni vigumu kutabiri jinsi wanyama watakavyoipokea watakapokuwa gizani mchana.Wanyama hutegemea saa ya kibaiolojia ya saa 24 ili kudhibiti tabia za kila siku kama vile kulala, kutafuta chakula na kuwinda. Jinsi kupatwa kwa jua kunavyovuruga taratibu hizi zilizokita mizizi haijagunduliwa kwa kiasi, kwani matukio ya ulimwengu ni matukio adimu ambayo hutokea popote kutoka takribani mara moja kila baada ya miaka 400 na pia si wanyama wote hutenda kwa njia sawa.

“Nuru ni ishara kubwa inayoathiri kila kitu kuanzia mimea hadi wanyama,” anasema Cecilia Nilsson, mwanaikolojia wa tabia katika Chuo Kikuu cha Lund cha Sweden. "Kama wanabiolojia, hatuwezi kuzima jua, lakini kila mara, asili hutuzima."

Zaidi ya miaka 100 iliyopita, William Wheeler, mtaalamu wa wadudu wa New England, alijaribu wakati wa hali ya kutoweka kwa jua kwa kuweka matangazo kwenye magazeti ya eneo hilo na kuandikisha umma kurekodi mabadiliko katika tabia ya wanyama wakati wa kupatwa kwa jua mwaka 1932.

Amekusanya hadithi zaidi ya 500, ambazo aliweka chati ya mabadiliko ya ndege, mamalia, wadudu na mimea, ikiwa ni pamoja na bundi ambao walianza kupiga kelele na nyuki waliorudi kwenye mizinga yao.


Mnamo Agosti 2017, kupatwa kwa jua ambako kulizuia miale ya jua kwa dakika mbili na sekunde 42 kuliwaruhusu wanasayansi kurudia jaribio hili.

Wakati huu, tukio lilikuwa na matokeo ya kushangaza zaidi. Giza lilipokaribia, twiga walikimbia kwa woga, kobe waliopanda bustani ya wanyama huko Carolina Kusini, na nyuki waliacha kulia huko Oregon, Idaho na Missouri.

Kupatwa kwa jua kulifuata mnamo Aprili 8, udadisi ulichochewa tena. Kando ya ukanda mwembamba wa ardhi, kutoka Mexico hadi jimbo la Maine la Marekani, wanasayansi watafuatilia kwa karibu njia ya kupatwa kwa jua, na wanawahimiza watu kutambua tabia yoyote ya ajabu.

"Kulikuwa na wasiwasi kwenye bustani ya wanyama."

Adam Hartstone-Rose, mwanasayansi anayefanya kazi katika Mbuga ya Wanyama ya Riverbanks huko Carolina Kusini, awali alifikiri wakazi wa mbuga za wanyama hawatasumbuliwa na kupatwa kwa 2017, na kupuuza kwani ingepeitia mawingu au dhoruba ya mvua.

Licha ya hayo, watafiti waliofunzwa na vikosi vya wanasayansi walikusanyika kwenye bustani ya wanyama ili kuchunguza viumbe 17 kabla na baada ya kupatwa kwa jua.

"Ilikuwa hali ya kushangaza kwa sababu bustani ya wanyama ilikuwa imepitia hali ya wasiwasi mwingi siku hiyo," asnaema. "Kulikuwa na maelfu ya watu, na kila mtu alifurahi."

Hartstone-Rose anasema zaidi ya robo tatu ya wanyama waliotazamwa walikuwa na athari ya wazi kutokana na tukio la "kushangaza" na "kubadilisha maisha".

Mitindo mingi iliainishwa katika sifa nne: wanyama walio na tabia ya kawaida, wale ambao walifanya mazoezi yao ya jioni, wale walioonesha wasiwasi au wale walioonesha tabia mpya.

Wanyama wengine, kama vile dubu wa grizzly, hawakujali kabisa kuhusu tukio la nadra la ulimwengu. "Walikuwa wamelala na wamestarehe katika muda wote wa tukio," anasema Hartstone-Rose. "Kwa ujumla, mtu aligeuza kichwa chake kuonesha kwamba anajali sana," anaongeza.

Ndege wa usiku, kwa upande mwingine, walionekana kushangaa sana. "Wakati wa mchana, Tawny Frogmouths hujitahidi wawezavyo kuonekana kama gogo linalooza," asema Hartstone Rose. "Hao ni ndege waliofichwa na kisha kumwaga nguo zao usiku kutafuta chakula." "Hivyo ndivyo walivyofanya wakati wa kilele cha kupatwa kwa jua," Hartston-Rose anaongeza. "Jua lilipotokea tena, ndege walirudi kwenye nafasi yao ya shina la mti."

Kwa bahati mbaya, wanyama wengine walionesha dalili za wasiwasi na dhiki wakati wa kupatwa kwa jua.Hartstone Rose anasema kwamba twiga, ambao "kawaida ni wanyama walio lege lege sana," walianza kukimbia kana kwamba wamemwona mwindaji au gari porini.

Hiki ndicho kilichotokea kwa twiga katika Bustani ya Wanyama ya Natchville huko Tennessee, ambao walipata wasiwasi na kuanza kukimbia baada ya kupatwa kwa jua.

Ingawa bustani ya wanyama ilikuwa mazingira ya kipekee ya kuona wanyama wadogo tofauti wakiitikia kupatwa kwa jua, kulikuwa na matatizo. "Kupatwa kwa jua kunasisimua, kwa hiyo watu walikuwa na sauti nyingi," asema Hartston Rose. Anasema kuwa moja ya maswali kuhusiana na wanyama walioathiriwa na kupatwa kwa jua ni: je, walikuwa wakiingiliana na kupatwa kwenyewe au kuwaona wanadamu wakiingiliana na kupatwa kwa jua?

Porini

Mbinu iliyopitishwa zaidi ilitokana na data kutoka kwa takribani vituo 143 vya hali ya hewa, vinavyoanzia mashariki hadi pwani ya magharibi ya Marekani.

"Tuna mtandao huu ambao daima unafuatilia anga, na ni fursa nzuri ya kuchunguza matukio haya adimu kwa viwango vikubwa," anasema Nelson, ambaye aliongoza utafiti huo.

Wanasayansi walijiuliza ikiwa ndege wa usiku wangekimbilia angani, wakifikiri kwamba badiliko la nuru lilikuwa ni kutua kwa jua. Hata hivyo, ni vigumu kuona ndege wakiruka wakati wa giza la kupatwa, ambapo vituo vya hali ya hewa huingia.

Jua linapotua, shughuli angani kwa kawaida hufikia kilele chake, ndege wanapoanza kuhama usiku. Lakini je, kipindi kisicho cha asili cha giza katikati ya mchana kinaweza kuwa ishara ya mazingira?

"Tulichoona ni kupungua kwa idadi ya ndege angani," Nelson asema. Ndege wengi walitua au kuacha kuruka wakati wa kupatwa kwa jua.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI