Basi la Kampuni ya Lujiga Express lililokuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea Mwanza limepata ajali eneo la Malendi wilayani Iramba Mkoa wa Singida na kusababisha vifo vya watu saba.
Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda amesema ajali hiyo imesababisha vifo vya watu saba huku wanaume wakiwa sita.
Amesema majeruhi wanane waliotokana na ajali hiyo wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Igunga na Hospitali ya Kiomboi wakipatiwa matibabu zaidi.
Kwa taarifa zaidi endelea kufuatilia www.matukiodaimamedia.co.tz…
0 Comments