NA. MATUKIO DAIMA APP
WAZIRI wa Ardhi na Maendeleo ya makaazi Zanzibar, Dk. Rahma Kassim Ali, amesema, Tanzania lipo eneo kubwa linalofaa kwa makaazi ingawa nyumba zilizopo ni chache zikilinganishwa na mahitaji.
Aliyasema hayo alipokuwa akifungua mkutano wa wadau wa mikopo ya nyumba za makaazi ulioandaliwa na benki ya CRDB yaliyofanyika katika ukumbi wa Golden Tulip uwanja wa ndege mjini Unguja.
Alisema kumekuwepo kwa changamoto nyingi zinazowakwamisha wananchi kujenga nyumba bora ikiwemo za kiutamaduni, kiimani na kiuchumi ambapo alisema kuwepo kwa mkutano huo unaweza kuzibainisha na kuweka mkakati wa kuzishughulikia.
Aidha alisema serikali imechukua hatua kadhaa na inaendelea kubuni namna ya kurahisisha urasmishaji na umilikishaji wa ardhi kwa wananchi ili wapate hati za maeneo yao ili kukidhi vigezo vya kupata mkopo wa nyumba kutoka benki.
Alisema kadri Zanzibar inavyokuwa na makaazi bora ndivyo tunavyowaandaa wananchi kwa maendeleo makubwa zaidi, hivyo, alisema mkutano huo utajadili kwa kina namna ya kuondoa vikwazo vilivyopo na kuwawezesha Watanzania kuishi maisha bora.
Hata hivyo, alipongeza benki hiyo kwa kujitolea ili kuona kuona changamoto zilizokuwepo zinaondoka na wananchi wanaweza kupata makaazi yaliyokuwa bora zaidi.
Sambamba na hayo, aliomba Kampuni ya Mikopo ya Nyumba Tanzania (TMRC) kuzijumuisha benki tatu zilizobaki ili nazo ziwe zinatoa mikopo ya nyumba ambapo taarifa zilizopo hivi sasa zinaonesha ni benki 31 tu ndizo zinafanya hivyo kwa sasa ila sokoni zipo 34
"Fanyeni hivyo ili mwananchi asikose huduma pindi atakapoitaka lakini, kiukweli nawapongeza kwa kazi nzuri mnayoifanya" alisema.
Waziri Rahma alifahamisha kuwa Mwaka jana, benki zote 31 zinazotoa mikopo ya nyumba zilikopesha jumla ya shilingi bilioni 587.24 ingawa kiasi hiki kilipanda kwa asilimia 10 ikilinganishwa na kilichotolewa mwaka 2022.
Mapema, Kaimu Mkurugenzi wa wateja wadogo na wa kati wa Benki ya CRDB, Stephen Adili, aliomba serikali iweze kurahisisha upatikana wa hati miliki wa viwanja ili kuweza kupata umiliki kwa urahisi.
Aidha aisema benki hiyo imekuwa kainara ya kuona wananchi wa Afrika mashariki ili kuona wananchi wanaendelea kuishi katika makazi yaliyokuwa bora zaidi.
Aidha alisena wamekuwa na mikutano mbalimbali na wananchi ili kuona ili changamoto zilizopo ikiwemo upatikanaji wa hatimiliki ili kuona wananchi wanapatiwa hatimiliki na kueleza kuwa wamekuwa wakijenga nyumba kwa bei urahisi.
Alifahamisha kuwa benki hiyo imeanza safari yake ya kutafuta suluhisho la makaazi ya wananchi tokea mwaka 2012 lengo ni kuona mtanzania anakuwa na makaazi yaliyokuwa bora ambayo yanamuwezesha kayoka kuishi sehemu yenye heshima kwake na kwa familia.
Hivyo, aliahidi kuendelea kushirikiana na serikali kuona wananchi wanaendelea kuishi katika nyumba inayokidhi katika mahitaji yake.
Nao wadau wamepongeza wazo lilotolewa na Benki kwani lengo lao ni kuona wananchi wanaendelea kupata makaazi yaliyokuwa bora kwao na kwa familia zao.
Mkutano huo wa siku moja ulioandaliwa na Benki ya CRDB umewashirikisha wadau mbalimbali ikiwemo Taasisi ya TMRC, ZHC,ZSSF, FUMBA UPTOWN,2410.
0 Comments