Header Ads Widget

MBUNGE PATRICK NDAKIDEMI AGAWA GESI JIMBONI KWAKE.

 



NA WILLIUM PAUL, MOSHI.


MBUNGE wa Jimbo la Moshi Vijijini Prof Patrick Ndakidemi* leo tarehe amewaalika Viongozi wa Matawi wa Chama cha Mapinduzi CCM(Wenyeviti wa Matawi, Makatibu wa Matawi na Waenezi wa Matawi) wote katika Jimbo la Moshi Vijijini katika ukumbi wa CCM mkoa ambapo aliwakabidhi mitungi ya Gesi kwa ajili matumizi ya nyumbani ikiwa ni pamoja na kuwapa Elimu juu matumizi yake na umuhimu wa kutumia gesi. 



Hafla hiyo ilihudhuriwa na Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya akiwemo Kaimu Katibu wa CCM Wilaya ya Moshi Vijijini Andrew  Mwandu, Katibu wa UVCCM Wilaya ya Moshi Vijijini, Pantaleo Melkiory pamoja na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Wilaya na Mjumbe wa Baraza la Jumuiya ya Wazazi mkoa Emanuel Mlaki. 



Akizungumza katika hafla hiyo fupi Mbunge aliwaeleza mambo mbali mbali yaliyofanywa na Serikali chini ya Rais Dkt Samia Suluh Hassan katika kila Kata ndani ya Jimbo la Moshi Vijijini na hivyo kuwataka viongozi hao kuendelea kusemea mazuri yaliyofanywa na Serikali pamoja na Viongozi wengine. 



Aidha, Viongozi hao kwa nyakati tofauti wamemshukuru sana Mbunge kwa kuwakumbuka kwani hawajawahi kukumbukwa kwa kipindi kirefu na kumuahidi wataendelea kumpa ushirikiano na kumuunga mkono ili maendeleo katika Jimbo la Moshi Vijijini yaendelee kuja kasi na Viwango.



Mwisho. . 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI