MBUNGE wa viti maalum mkoa wa Lindi kupitia chama cha Mapinduzi CCM Maimuna Pathan amewataka watanzania kujiunga kwenye bima ya NHIF kwa kuwa ndio mkombozi wa huduma za afya kwa wananchi wote Tanzania.
Akizungumza na waandishi wetu Mbunge Maimuna alisema kuwa watanzania wanatakiwa kumuunga mkono Rais Dr Samia suluhu Hassan kwenye juhudi za kuboresha afya kwa watanzania na wasio watanzania.
Maimuna alisema kuwa wananchi wanapaswa kupuuza madai ya wanaharakati wanapinga uwepo wa bima ya afya ya NHIF ambayo ndio mkombozi wa wananchi.
Alisema kuwa kila kona ya nchi ya Tanzania kimejengwa hospitali za wilaya ambazo zinatoa huduma kwa ubora unaotakiwa kama ambavyo swali zilikuwa zinatolewa kwenye hospitali za watu binafsi hivyo wananchi rudi kupata huduma ya afya kwenye hospitali za serikali.
Watanzania wenzangu twendeni tukapata huduma za kiafya kwenye hospitali za serikali, turudi nyumbani kumenoga mama Dr Samia suluhu Hassan anaupiga mwingi
0 Comments