Header Ads Widget

MATUMIZI YA HUDUMA ZA FEDHA ZANZIBAR YAMEKUWA KWA ASILIMIA 82 NA KIWANGO CHA UTEGEMEZI KWA WATU BADO KIPO JUU


NA THABIT MADAI, ZANZIBAR -MATUKIO DAIMA

RIPOTI ya Mpya ya masuala ya Fedha (Finscope) Tanzania 2023 ripoti  mahususi ya Pili ya Zanzibar imezinduliwa rasmi  na Makamu wa Pili wa Rais  Hemed Suleiman Abdulla kwa niaba ya Rais wa Zanzibar Dk.Hussein Ali Mwinyi ambayo inaonesha Mahitaji, matumizi na upatikanaji wa  huduma jumuishi za  fedha yameongezeka kutoka Asilimia 45 mwaka 2017 hadi asilimia 82 mwaka 2023.

Aidha ripoti hiyo inaonesha kuwa, Zanzibar  ina idadi kubwa ya watu wanaoweka akiba ya Fedha huku Matumizi ya Bima yakiwa madogo ukilinganisha na maeneo mengine Tanzania.

Hata hivyo ripoti hiyo inaonesha kiwango cha utegemezi kwa watu bado kipo juu Visiwani Zanzibar.

Akihutubia Wananchi mara baada ya uzinduzi wa ripoti hiyo, Makamu wa Pili wa Rais amesema kuwa, Serikali inaridhishwa na matokeo ya utafiti huo ambao unaonesha hali ya matumuzi jumuishi ya huduma za fedha yameongezeka kwa asilia 82 mwaka 2023 kutoka 45 mwaka 2017.

Amesema kuwa, Tahiti zinaonesha uwiano wa ujumuishaji wa  fedha kwa jinsia zote umepungua kwa asiliamia kubwa huku uchumi wa  Wanawake ukiongeza na kuondokana na utegemezi.

Aidha kulingana Mafanikio ya utafiti huo Serikali imejipanga kuhakikisha kuwa maendeleo ya sekta ya fedha ba huduma za fedha jumuishi zinaimarika zaidi.

Amesema, sote ni mashahidi wa namna ambavyo matokeo ya Utafiti wa Finscope Tanzania 2017 ripoti ya Zanzibar, yalivyosaidia michakato mbalimbali ya kuboresha na kuongeza upatikanaji wa bidhaa na huduma jumuishi za fedha kwa wananchi. 

"FinScope imesaidia watunga sera kufanya mapitio ya sera kikamilifu, kuunda zana za ufuatiliaji kwenye sekta ya fedha, na kuweka mikakati ya kuongeza ustawi na huduma jumuishi za fedha. Kwa wadau wa sekta binafsi, FinScope imewasaidia kubuni bidhaa na huduma za fedha  zinazoendana na soko na kukidhi mahitaji ya wateja."

Mapema Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar  Sada Mkuya amesema kuwa utafiti huo ni njezo muhimu  inayoweza kutumika na wadau wote kama Dira ya kufanya maamuzi sahihi kwa maendeleo ya nchi.

"Utafiti huu tutauchukua na kuufanyia kazi kwa kuusambaza kwa wadau wote ili wachukue hatua stahiki," ameeleza.

 Ameeleza kuwa utafiti huo unasaidia kubuni bidhaa za fedha zinazoendana na soko na kukidhi mahitaji ya wateja

Utafiti huo hupima mahitaji, upatikanaji na matumizi ya huduma zafedha Unguja na Pemba.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI