Mke wa Rais wa Zanzibar, Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) Mhe.Mama Mariamn Mwinyi ameitaka jamii kuchukua jitihada za makusudi kuhakikisha wanaepuka magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo Kisukari, Moyo, shinikizo la damu na mengineyo ili kupunguza mzigo wa gharama za matibabu kwa familia na Serikali.
Mama Mariam Mwinyi amesema hayo akifunga kambi ya siku tano ya Matibabu ya "Afya Bora, Maisha Bora" iliyohudumia zaidi ya wananchi 5000 chini ya Taasisi ya ZMBF sambamba na kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika Viwanja vya Mkwajuni Wilaya ya Kaskazini A Mkoa wa Kaskazini Unguja tarehe: 8 Machi 2024.
Aidha Mama Mariam Mwinyi amewahimiza wananchi umuhimu wa kuzingatia lishe bora hususani wanawake walio katika umri wa kubeba ujauzito ili kupunguza hatari ya kupata safura, utapia mlo na udumavu kwa watoto.
Vilevile, Mama Mariam Mwinyi ameshiriki katika matembezi yanayoitwa Mariam Mwinyi Walkathon kuanzia Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja mpaka Viwanja vya Mkwajuni.
0 Comments