Header Ads Widget

MADIWANI WATAKA JWTZ LISHUGHULIKIE 'KAMCHAPE'

 

Madiwani wa halmashauri ya wilaya Kasulu
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, Eliya Kagoma

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

Madiwani katika halmashauri ya Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma wameiomba serikali kulikabidhi  jeshi la polisi kazi ya kupambana na vitendo vya waganga matapeli maarufu kama Kamchape kutokana na vitendo vya waganga hao kuleta athari kubwa kwa jamii.

Madiwani hao wametoa kauli hiyo katika kikao cha robo ya pili cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha 2023/2024, ambapo wamependekeza kuwa kwa hali ya sasa ni vizuri jeshi la wananchi likaongezwa kwenye kazi hiyo ili kusaidiana na jeshi la polisi ambao kwa muda mrefu ndiyo waliokuwa wakisimamia kupambana na waganga hao.

Pendekezo hilo la madiwani linakuja baada ya hoja ya Diwani wa Kata ya Bugaga,  Hitla Joseph  kutoa hoja ya dharura kuhusu suala hilo la Kamchape ili lijadiliwe huku akieleza madhara yaliyosababishwa na Kamchape au kwa jina lingine ‘Lamba Lamba’.

Diwani huyo akizungumza huku akitoa mifano alisema kuwa kata ya Kurugongo mchungaji alipigwa na wananchi waliofuatana na waganga hao matapeli na mali zake kuharibiwa kwa madai ya kuwa ni mchawi ambapo pia katika kata hiyo mama mmoja alimwagiwa maji ya moto kwamba ni mchawi hiyo kuathirika kimwili na kiakili

Baada ya kutoa hoja hiyo kuwasilishwa Diwani wa kata ya Rungwe Mpya Abeli Jonas Kaja alisema kuwa polisi wamefanya kazi kubwa kupambana na waganga hao matapeli lakini kwa hali ya sasa wamezidiwa hivyo ni vizuri JKT na jeshi la wananchi wakaingia kazini kuisadia polisi kupambana na hali hiyo.

Kufuatia mapendekezo hayo  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, Eliya Kagoma akahitimisha hoja hiyo aliwaomba madiwani kupitia baraza hilo  kuridhia halmashauri kuichangia mafuta Polisi ili kuzidisha mapambano dhidi ya waganga hao matapeli ‘Kamchape’.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya Kasulu,  Emmanuel Ladislaus aliliambia baraza hilo la madiwani kwamba hoja iliyoibuliwa na madiwani katika baraza hilo la kuichangia polisi mafuta kwa ajili ya kupambana na waganga matapeli inawezekana.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS