Na Mwandishi Wetu.
GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Emmanuel Tutuba amewahimiza wamiliki na waendeshaji wa Hoteli zenye hadhi ya nyota Tatu hadi Tano Zanzibar kuchangamkia fursa ya kupata leseni na kuanza kutoa huduma za kubadilisha fedha za kigeni ili kupunguza soko haramu la ubadilishwaji wa fedha.
Wito huo ameutoa leo katika mkutano na baadhi ya Wamiliki na waendeshaji wa Hoteli zinazopokea watalii nchini uliofanyika katika Ofisi ndogo za Makao Makuu ya Benki Kuu Gulioni Zanzibar ambapo amesema kuwa, kutokana na Mabadiliko ya Sheria inatoa fursa kwa Hoteli kutoa huduma za kubadilisha fedha jambo ambalo linasaidia kuondoa usumbufu kwa wateja wao.Aidha Gavana ameeleza kuwa msingi wa kufanya marekebisho ya Kanuni umetokana na utafiti uliofanywa na Benki Kuu na kugundua urasismishwaji wa maduka ya fedha za kigeni haukuhusisha hoteli na kuchochea soko kubwa la biashara haramu za kubadilisha fedha za kigeni.
Mkutano huo uliohudhuriwa na wamiliki na waendeshaji wa Hoteli unatokana na hatua iliyochukuliwa na Benki Kuu ya kurekebisha kanuni ya maduka ya kubadilisha fedha za kigeni ambapo Sheria hiyo inaruhusu hoteli za kitalii kupata leseni za kutoa huduma za kubadilisha fedha za kigeni kwa wateja wao.
0 Comments