Header Ads Widget

RUNALI YAGAWA MBEGU ZA UFUTA NA ALIZETI BURE KWA WANACHAMA WAKE

NA HADIJA OMARY Ili kuongeza uzalishaji wa zao la Ufuta na kufanya uhamasijaji kwa  wakulima kulima zao la Alizeti chama Kikuu cha ushirika RUNALI kinachohudumia wakulima wa Wilaya za Ruangwa Nachingwea na Liwale Mkoani kimegawa mbegu za mazao hayo bure  kwa wakulima wanachama wakeAkizungumza wakati wa ugawaji wa Mbegu hizo leo February 13 uliofanyika katika ofisi za Chama hicho Wilayani Nachingwea  Mkuu wa Wilaya ya hiyo Mohamed Moyo  aliwataka viongozi wa vyama vya msingi AMCOS kwenda kuzigawa Mbegu hizo kwa wakulima waliokusudiwa sambamba na kuweka utaratibu rafiki katika ugawaji wa mbegu.Hata hivyo moyo pia aliwasisitiza wakulima  kuwatumia na kufuata maelekezo ya  maafisa Ugani wakati wanapoenda kuandaa mashamba yao.Meneja Mkuu wa chama hicho Jahida Hassan amesema mbegu hizo zimegawa  ni tani 2 za ufuta na tani 4 za Alizeti na zimegaiwa kwa kuzingatia maeneo yenye uzalishaji mkubwa wa ufuta, maeneo ambayo hayastawi mazao mbadala  kwa alizeti pamoja na maeneo yaliyopata athari ya mvua na wanyama waalibifu kama tembo"Kama mnovyojua mwaka huu mvua zimekuwa nyingi sana kuna maeneo kuna maeneo ambayo yameathiriwa na mvua wakulima walipanda Ufuta lakini umezolewa na mvua kwa hivyo tumezingatia pia hayo maeneo mfano kama namapwia, lionja hayo ni maeneo yaliyoathirika na mvua na tembo"Kwa upande wake Afisa ushirika Mkoa wa Lindi projestus Paschal amewapongeza Runali kwa kutoabegu hizo kwa wanachama wake ambapo amesema itendo  ni utekelezaji wa msingi wa saba wa ushirika ambao unawataka vyama pindi wanapokusanya tozo wahakikishe wanarudisha kwa jamii Mwenyekiti wa  chama kikuu cha ushirika RUNALI Odas Mpunga amesema hiyo ni mara ya pili kwa chama cha Chao kugawa mbegu kwa wakulima wao ambapo kwa sasa wameanza kuona tija baada ya msimu uliopita wa 2022/2023 ambapo uzalishaji ulikuwa tani elfu 16 lakini baada ya kugawa mbegu mwaka 2023/2024 uzalishaji ulipanda hadi kufikia hadi tani elfu 23 na sasa matarajio yao kuongeza mpaka kufikia tani elfu 30 kwa msimu ujao wa 2024/2025Kwa upande wao wakulima akiwemo Shamsia Naluchonga na Kasim Lada walikishukuru chama chao kwa kuwapatia mbegu hizo bure ambapo walisema mbegu hizo zitawasaidia kuongeza uzalishaji katika mazao hayo

 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI