Header Ads Widget

MUME AUA MKE AJINYONGA HADI KUFA


VIDEO BOFYA LINK HII 

MUME AUA MKE AJINYONGA HADI KUFA



Na Fadhili Abdallah,Kigoma

 

mkazi wa mtaa Gemu kata ya Mwanga Kusini Manispaa ya Kigoma Ujiji Rashidi Hussein Mkayaga amejinyonga kwa kutumia kilemba cha kiume cha kuvaa kichwani  muda mfupi baada ya kumuua mke wake Bernadeta Cosmas kwa kumnyonga shingo hadi kufa katika kile kinachoelezwa kutokea mgogoro baina ya wanandoa hao.

 

kaka wa marehemu Magdalena anayejulikana kwa jina la Isack Cosmas akizungumza na waandishi wa Habari eneo tukio alisema kuwa siku ya tukio majira ya saa tatu asubuhiwa  alipigiwa simu na dada yake Bernadeta Cosmas akimtaka afike nyumbani kwa dada yake  kwani alikuwa na jambo muhimu alitaka kuongea naye.

 

Alisema kuwa kutokana na msisitizo huo alilazimika kuacha shughuli zake na Kwenda mtaa wa Gemu alipo dada yake ambapo alifika na kukuta yupo kwa mwenyekiti wa mtaa hivyo alimweleza kilichotokea ikiwemo kipigo alichopata kutoka kwa mume wake baada ya Kwenda nyumba moja ya Jirani kuchukua nyaya ya TV ambapo mume wake alikuwa ameuza hivyo alimpiga na kumkaba  na waya wa umeme na kunusurika kufa.

 

Katika maongezi yao Kaka huyo wa marehemu alisema kuwa dada yake alimweleza kuwa amemtaka mume wake ampe talaka yake waachane kila mtu aishi Maisha yake na ndipo kaka yake akamweleza kuwa suala hilo itabidi waende dawati la jinsia polisi kupata ushauri na hatua za kuchukua kukabiliana na hali hiyo.

 

Aidha Isack alisema kuwa  akiwa na dada yake alifika nyumbani kwa shemeji yake na kumkuta shemeji yake yupo hapo nyumbani ambapo katika mazungumzo yake Shemeji huyo aliahidi kwamba mgogoro umeisha na yupo tayari kuishi na mke wake hivyo alimuacha dada yake nyumbani hapo akiwa na mumewe na kuondoka.

 

Aidha alisema kuwa jioni alipiga simu kumtafuta dada yake lakini simu ilikuwa ikiita bila kupokewa na ilipofika saa moja usiku alikwenda kwa dada yake lakini alikuta mlango wa nje ukiwa umefungwa na kufuli hivyo aliondoka lakini hata aliporudi saa saba usiku alikuwa hali iko hivyo hadi asubuhi walipovunja mlango na kugundua dada yake ameuawa.

 

Mwenyekiti wa Mtaa Gemu,Buswalu Mulumbu Mkama  akizungumzia na waandishi wa Habari eneo la Tukio hilo alisema kuwa chanzo cha tukio hilo ni mgogoro uliotokea siku za nyuma ambapo Mke wa marehemu alifika kwa mwenyekiti na kutoa taarifa ya vitendo vya  mume wake kuchukua vitu vya ndani na kuuza ambapo mara kadhaa kesi za wanandoa hao zilikuwa zikipelekwa kwake kwa ajili ya usuluhishi.

 

Mwenyekiti huyo alisema kuwa siku moja kabla tukio marehemu alilala nyumbani kwake baada ya kukimbia nyumbani kwa mume wake kufuatia kipigo alichopata kwa mume wake ambapo katika tukio hilo alinusurika kuuawa baada ya kukabwa shingo na waya wa umeme hivyo alipopata nafasi ya kuchomoka alikimbia na kukimbilia kwa mwenyekiti wa mtaa ambapo alilala hadi siku ya tukio ambapo kabla tukio kaka wa mareheme alipokuja kumchukua ndugu yake.

 

 

Uchunguzi wa awali wa tukio hilo unaonyesha kuwa Marehemu Rashidi Hussein alimnyonga mke wake kwa mikono hadi kumuua na baadaye kutoka nje ambapo alifunga mlango kwa nje na kurudi ndani kupitia dirishani ambapo alifunga milango yote na madirisha na yeye kujinyonga kwa kitambaa cha kichwani.

 

Mtoto wa marehemu, Hussein Rashidi akieleza tukio hilo alisema kuwa kumekuwa na ugomvi wa mara kwa mara wa wazazi wake usiku mmoja kabla ya tukio walilala kwa Mwenyekiti wa mtaa baada ya baba yake kumpiga mama yake na kumuumiza.

 

Kwa sasa miili yote miwili imehifadhiwa kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa Kigoma maweni wakati uchunguzi wa tukio hilo ukiendelea.

 



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS