Header Ads Widget

MADIWANI NJOMBE DC WALALAMIKIA UBOVU WA BARABARA

 

Meneja wa Tarura wilaya ya Njombe Mhandisi Costantine Ibengwe

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Njombe Mhe.Valentino Hongoli

xxxxxxx

Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE

Wakati Mvua kubwa zikiendelea kunyesha na kuharibu miundombinu mbalimbali ikiwemo ya Barabara Madiwani wilayani Njombe wamelalamikia hali mbaya ya barabara kwenye kata zao na kwamba hivi sasa kuna baadhi ya maeneo shughuli za usafirishaji zimetatizika pakubwa.

Katika kikao cha baraza la madiwani cha kupitisha Rasimu ya bajeti ya mwaka wa fedha ujao wa 2024/2025 kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 33 yamesomwa pia makadirio ya bajeti ya wakala wa barabara Tarura wilaya ya Njombe kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 2.


Pamoja na Rasimu hiyo ya Tarura lakini baadhi ya madiwani akiwemo Isaya Myamba,Roida Wandelage na Vasco Mgunda wamelalamikia adha wanazopata wananchi wao kutokana na   uharibifu wa barabara katika kipindi hiki cha mvua.

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Njombe Valentino Hongoli anataka ushirikiano wa karibu na wakala huo ili iwe rahisi kuwasimamia wakandarasi wanaotekeleza miradi mbalimbali.

Akitolea ufafanuzi wa hoja mbalimbali za madiwani juu ya ubovu wa barabara hivi sasa,Meneja wa wakala wa barabara za mijini na vijijini TARURA Wilaya ya Njombe Mhandisi Costantine Ibengwe amekiri kuwapo kwa changamoto hizo na kwamba hatua za dharura zinaendelea kuchukuliwa wakati wakisubiri mvua zipungue.

  

Baadhi ya maeneo nchini yameharibiwa vibaya na mvua zinazoendelea kunyesha kwa kusombwa kwa madaraja,Nyumba na hata miundombinu mingine ikiwemo ya Elimu na Afya.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI