Header Ads Widget

BREAKING NEWS:MSAFARA WA BITEKO WAPATA AJALI IRINGA

 






Taarifa za hivi punde gari moja wapo lenye namba za usajili aina ya Toyota lenye namba za usajili  STL 9035  lililokuwa kwenye Msafara wa N/Waziri mkuu limepata ajali na mtu mmoja anahofiwa kufariki Dunia Ajali imetokea eneo la Mlolo Iringa vijijini barabara kuu Iringa -Mbeya.

Mwandishi wa Matukio Daima Media amefika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa majira ya Saa 3:45 usiku wa Leo Alhamis February 22 /2024 na kushuhudia Magari zaidi ya 7 yaliyokuwepo kwenye Msafara huo yakiwa eneo la OPD huku nyuso za watu waliokuwepo eneo hili zikiwa za huzuni .

Mmoja kati ya madereva wa Magari hayo alizungumza na mwandishi wa Matukio Daima App pasipo kutaja jina lake alisema gari Hilo lilikuwa limepakia maofisi zaidi ya watatu na wakati likipata Ajali alikuwa akishuhudia kwani lilikuwa mbele yake kwenye Msafara huo.

Hata hivyo alisema mtu mmoja aliyekuwa amekaa mbele ndie aliyepoteza maisha na mwili wake umepelekwa chumba Cha kuhifadhi maiti huku Dereva na afisa mmoja wamejeruhiwa  .

Hata hivyo jitihada za kumpata mganga mfawidhi wa Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Iringa Dkt Alfred Mwakalebela hazikuzaa matunda baada ya simu yake kuita bila kupokelewa.

RPC Iringa Allan Bukumbi alipotafutwa Kwa Njia ya simu amethibitisha kutokea Kwa Ajali hiyo japo alisema bado hajajua kama Kuna Kifo ama lah .

"Ni kweli Ajali imetokea Kuna gari lilifuatana na Msafara huo limepata ajali ila halijulikani ni la idara gani ila RTO amekwenda Kufuatilia nitakupatia taarifa kamili usiku huu "alisema RPC Bukumbi  

Msafara wa Naibu Waziri mkuu na Waziri wa Nishati Mhe Biteko ulikuwa ukitokea kuwasha umeme Kijiji Cha Mkangwe kata ya Idunda  na kufanya vijiji vyote 360 ndani ya mkoa wa Iringa kupata umeme .

Endelea kufuatilia APP YA  MATUKIO DAIMA kwa habari zaidi .



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS