Header Ads Widget

WANANCHI PUUZIENI MAANDAMANO YA CHADEMA

 




Na Hamida Ramadhani Matukio Daima App Dodoma

WENYEVITI wa Vyama vya Upinzani Dodoma wametoa wito kwa Watanzania na wakazi wa Dodoma kupuuza kauli ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Freeman Mbowe Kuitisha  maandamano yanayotarajiwa kufanyika Januari 24 mwaka huu kwa kushinikiza  Serikali kuzingatia maoni na mapendekezo ya wadau wa uchaguzi nchini. 

Miswada hiyo ni Muswada wa sheria ya uchaguzi wa Rais, Wabunge, na Madiwani wa mwaka 2023 Muswada wa sheria ya tume ya taifa ya uchaguzi wa mwaka 2023 na Muswada wa Sheria ya malekebisho ya sheria ya vyama vya Siasa ya mwaka 2023.



Wameyasema hayo leojijini hapa wakati walipokuwa Wakizungumza na waandishi wa habari huku wamewataka wananchi na wanachama wote kwa ujumla kupuiza maandamano hayo na kuendelea na kazi zao za ujenzi wa taifa kwa kuwa mchakato bado unaendelea bungeni. 

Akiongea kwenye mkutano huo Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Dodoma Yohana Mussa amesema Maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) waliyoyaita ya Amani Ukweli ni kwa MBA Ndani yake Maandamano haya yatakuwa sio ya Amani. 

"Sisi kama Chama cha ACT Wazalendo na wenyeviti wenzangu tunaamini maoni yetu yatazingatiwa na wabunge kwa kuwa tumeiona nia njema ya Rais Samian a Serikali Katika jambo ili, " Amesema.

Na kuongeza kusema "Kwanini Sisi Wenyeviti tusema Maandamano haya sio ya Amani, kwa Kuwa chama ichi kimeacha mchakato halali wa majadiliano na fulsa iliyotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan ya Maridhiano Kisiasa na kujenga umoja wa kitaifa lakini cha kushangaza MBOWE NA CHADEMA wanataka kuwaingiza watu barabarani kufanya maandamano katika nyakati hizi ambazo taifa letu linahitaji utulivu mkubwa, " Amesema Mwenyekiti huyo Mussa.



Naye Mwenyekiti wa Chama cha wananchi (CUF) Stephen Chitema  amewaka wabunge kuzingatia maoni yaliyotolewa kikao kazi  juu ya mabadiliko ya katiba kwani Jamboree hilo ni la muda mrefu na limekuwa likitumia fedha nyingi. 

Kuhusu maandamano ya tarehe 24 amesema Freeman Mbowe ameitisha maandamano ya wafuasi wake na wananchi, wakati ambao wananchi wapo mashambani wakiendelea na kilimo, 

"Kwa wito huu anataka wananchi watoke kwenye shughuri za kilimo waje mijini kuandamana hii sio sahihi, " Amesema

Amesema Mbowe anaitisha maandamano katika jiji la kibiashara dar uku akitambua juhudi zilizofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan kufungua frusa za uwekezaji na biashara katika jiji ilo.

"Lengo hapa sio maandamano ya Amani ila ni uharibifu wa juhudi za Mhe. Rais Katika Kuifungua Nchi

"Sisi Wenyeviti wa Vyama Vya Upinzani Tuliopo Makao Makuu ya Nchini Tunampongeza Rais Samia Suluhu Hassan Kwa Uamuzi Wake wa Kupeleka Bungeni Marekebisho ya sheria ya uchaguzi ambapo sasa, kamati ya kudumu ya bunge ya katiba na sheria chini ya mwenyekiti wake Joseph Mhagama imetoa fulsa kwa wadau mbalimbali kutoa maoni yao wakiwao CHADEMA nafasi kwa wadau kutoa maoni yao kila mmoja kwa nafasi yake,

Amesema kamati ya bunge ilitoa ushirikiano wa kutosha kwa wadau KIASI cha kutosha ilifikia baadhi ya wadau walipewa nafasi Zaidi ya mara moja kutoa maoni yao wakiwamo hawa wanaitisha maandamano

"Chama cha Chadema na Mwenyekiti wao Freeman Mbowe  imekuwa ni tabia yao kuacha michakato halali na kukimbilia kwa wananchi kujilizaliza, Sisi wenyeviti himala tunasema atuungi mkono maandamano hayo na tunalaani kwa nguvu kubwa ukiukaji huu wa maridhiano ya demokrasia yalianzishwa na Rais Samia Suluhu Hassan, " Amesema 



MWISHO.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI