Header Ads Widget

MADIWANI WAFANYA USAFI OFISI YA CCM WILAYA WAKATA KEKI KUMPONGEZA RAIS DKT SAMIA KWA SIKU YAKE YA KUZALIWA




NA SCOLASTICA MSEWA, MKURANGA

Baadhi ya Madiwani viti maalumu jimbo la wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani pamoja na Katibu wa UWT wilaya ya Mkuranga Nurati Mkandawile wamefanya usafi wa kuzunguka viwanja vya ofisi ya CCM wilaya ya Mkuranga ikiwa ni kushiriki kumpongeza Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika siku yake ya kuzaliwa.


Hafla hiyo fupi imefanyika katika Ofisi ya UWT Wilaya ya Mkuranga ambapo pia wamekata keki ya kumtakia maisha marefu yenye heri Rais Dkt Samia na kuwahusisha jumuhia ya Wazazi Wilaya waliokuwa kwenye mkutano wilayani hapo.


Aidha Nurati aliwataka Madiwani hapo Viti maalumu kwenda kuhamasisha akinamama kuchukua fomu za kuombea nafasi mbalimbali za uongozi katika chaguzi za serikali za mitaa na vitongoji muda utakapofika na kuwapa ushirikiano Wanawake watakaosubutu kuchukua fomu kuombea nafasi za uongozi ili washinde.


Hatahivyo pia Katibu huyo wa UWT Wilaya ya Mkuranga amewataka Madiwani Viti maalumu kuanza maandalizi ya kusubutu kuchukua fomu za kugombea nafasi ya udiwani wa Kata muda utakapofika.


Lakini pia Nurati amewataka Madiwani Viti maalumu hao kwenda kutembelea na kufanya mikutano na kuzungumza na akinamama kusikiliza kero za Wanawake katika Kata ,mitaa vitongoji, vijiji na mitaa yao .


Naye Diwani Viti maalumu Fatuma Kingwande amesema Madiwani hao wapo tayari mchana na usiku kwenda kukihudumia Chama na Wanachama wake ili CCM kikakubalike kwa Wanachama na kwa Wananchi pia.










Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI