Na Fadhili Abdallah,Kigoma
MAMLAKA ya mapato (TRA) mkoa Kigoma imetoa msaada wa magodoro 20,vyakula na vifaa mbalimbali kwa Watoto wenye changamoto ya usonji (OTISM) wanaohishi kwenye kituo cha kulelea watoto Bangwe Shelter Home cha mjini Kigoma.
Msaada huo ni sehemu ya kilele cha maadhimisho ya siku ya mlipa kodi ambapo misaada hiyo yenye thamani ya Zaidi ya shilingi milioni 2.5 inatokana na michango ya watumishi wa TRA mkoa Kigoma.
Meneja wa TRA mkoa Kigoma,Deogratius Shuma akiongozana na watumishi wa mamlaka hiyo mkoani Kigoma alikabidhi misaada hiyo kwa Watoto na uongozi wa kituo hicho akieleza kuwa misaada hiyo kidogo inatokana na namna watumishi hao wanavyoguswa na changamoto na uhitaji wa Watoto hao.
Shuma alisema kuwa hiyo ni sehemu moja ya msaada huo lakini pia waliweza kulipia matibabu ya Watoto 15 waliokuwa wamelazwa kwenye hospitali ya mkoa Kigoma Maweni kwa changamoto ya magonjwa mbalimbali.
Akipokea misaada hiyo kwa niaba ya Watoto na uongozi wa Bangwe Home Shelter Mkuu wa Shirika la Brothers of Charity Tanzania, Padre Chrisantus Rweikiza ameshukuru kwa msaada huo na kubainisha kuwa chakula na mahitaji ya kibinadamu ni changamoto kubwa katika kuendesha kituo hicho.
Kwa upande wake Mratibu wa kituo hicho,Padre Patrick Athanas alisema kuwa Pamoja na changamoto ya upatikanaji wa fedha kwa ajili ya uendeshaji wa kituo hicho alisema kuwa ubakaji kwa Watoto wenye usonji Tanzania kwa sasa limekuwa tatizo kubwa.
0 Comments