NA CHAUSIKU SAID, MATUKIO DAIMAAPP MWANZA.
Serikali kupitia Wizara ya mambo ya Ndani ya Nchi inaendelea kutekeleza dhamira yake ya kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazoikabili jeshi la zimamoto na uokoaji Nchini ikiwemo ujenzi wa miundombinu lengo likiwa ni kuimalisha ufanisi katika utendaji wa Jeshi hilo.
Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Kaspar Mmuya katika ufunguzi wa kikao Cha Baraza dogo la wafanyakazi wa jeshi hilo katika ukumbi wa Benki Kuu Mkoani Mwanza na kueleza kuwa kufanya hivyo kutawaongezea ufanisi wa utoaji wa huduma za zimamoto na uokoaji Kwa kufika kwenye maeneo ya matukio Kwa wakati.
Mmuya amesema kuwa Kwa upande wa vitendea kazi serikali imefanya ununuzi wa magari ya kuzima moto na uokoaji pamoja na magari ya utawala na itaendelea kufatilia upatikanaji wa fedha Kwa ajili ya ujenzi wa vituo vyote vya zimamoto na uokoaji na Miradi mingine.
"Hivi karibuni mwishoni mwa mwezi wa January 2024 mtapokea mitambo na magari 12 ya kuzimamoto kutoka Nchini Australia, pia serikali imefanikisha kupata mkopo wa masharti nafuu wa Dola za kigeni Million 100 kutoka Nchi za fedha za kiarabu Kwa ajili ya ununuzi wa vitendea kazi vya jeshi hilo ikiwemo mitambo ya kuzima moto" Alisema Mmuya.
Hata hivyo Mmuya ameeleza kuwa Kwa upande wa rasilimali watu serikali imetoka kibali Cha kuajiri askari wapya 200 na Wizara itaendelea kufanya ufuatiliaji ili kupata vibali zaidi vya ajira Kwa jeshi la zimamoto na uokoaji.
"Licha ya changamoto zilizotajwa, nalipongeza jeshi la zimamoto na uokoaji Kwa kuendelea kutoa huduma katika maeneo mbalimbali hapa Nchini sambamba na kutekeleza mpango wa kujengea uwezo wananchi" Alisema Mmuya.
Kamishina Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji John Masunga akitoa taarifa Kwa mgeni rasmi ameeleza kuwa Jeshi hilo limetengewa kiasi Cha sh Bil, 9.930 Kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi ya upanuzi na uboreshaji wa huduma, ikiwa ni pamoja na ununuzi wa magari matano (5) ya kuzimamoto na uokoaji, uendelezaji wa ujenzi wa vituo saba (7) katika Mikoa ya Songwe, Simiyu, Kagera, Njombe, Manyara, Katavi na Geita.
Masunga ameeleza kuwa mbali na mafaniko waliyoyapata bado zipo changamoto zinazoikabili jeshi hilo ikiwa ni pamoja na uhaba wa vifaa na vitendea kazi Kwa ajili ya utoaji wa huduma, uchache wa vituo vya zimamoto na uokoaji Nchini, upungufu wa maafisa na Askari Kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu ya jeshi .
Ujenzi holela katika maeneo mengi hususani mijini unaosababisha Askari kutofika Kwa urahisi wakati wa dharura za moto na majanga, uchache wa sehemu maalum za kujazia maji ya kuzima moto katika maeneo mengi ya mjini na uchakavu wa sehemu zilizopo.
Kaimu kamanda wa Jeshi la Zimamoto Mkoa wa Mwanza Kamila Raban ameeleza kuwa huduma za jeshi hilo zimeendelea kuimarika na askari kufanya kazi Kwa uweledi na kushiriki kwenye Miradi ya kimkakati.
0 Comments