MBUNGE wa Jimbo la Moshi vijijini wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro Prof. Patrick Ndakidemi ameipongeza serikali ya awamu ya sita kwa jinsi inavyotekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo ambapo hadi kufikia Julai mwaka huu Jimbo hilo limeshapokea Bilioni 35.1.
Prof. Ndakidemi ametoa kauli hiyo katika kikao cha Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi wilaya ya Moshi vijijini ambapo amekipongeza Chama hicho kwa kuisimamia vizuri Wabunge na serikali katika kuhakikisha utekelezaji wa Ilani unafanyika kwa vitendo.







0 Comments