Header Ads Widget

TPDC WAANZA UTEKELEZAJI WA MIRADI MITATU AMBAYO NI MAAGIZO YA NAIBU WAZIRI MKUU NA WAZIRI WA NISHATI DKT. DOTO BITEKO

Matukiodaima APP, Mtwara

Utekelezaji wa miradi mitatu waanza mtwara ambapo Shirika la Maendeleo ya Petrol Tanzania (TPDC) limesaini hati ya makubaliano na Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara, Jeshi la Polisi Tanzania na Wakala wa Barabara Tanzania(TANROADS) ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko alipotembelea mkoani hapa.


Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Mussa Makame alisema kuwa wanaingia mkataba huo ili kuanza utelekezaji wa maagizo yaliyotolewa na Naibu waziri mkuu Dkt.Doto Biteko ya kuhakikisha kuwa vijiji vinavyozunguka mradi wa gesi vinapata taa za barabarani, kituo cha afya na kituo cha Polisi vya kata.

Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mwanahamisi Munkunda  alisema kuwa miradi hiyo itasimamiwa ipasavyo na itakamilika kwa wakati ndani ya miezi mitatu tu ili kuruhusu wananchi wa eneo hilo kuanza kupata huduma mara moja.


"Hii miradi tutajenga majengo ya kisasa ili kituo cha afya kiweze kuwa na jengo la kujifungulia, upasuaji, maabara na majengo mengine muhimu lakini pia  tutaweka taa Madimba zitakuwa 30 , Mngoji zitakuwa 29  na Msimbati zitakuwa 57”alisema Munkunda

Mwenyekiti ya Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara  Selemani Nampanye amesema kuwa bado wanamahitaji makubwa ya huduma za kijamii utekelezaji wa ujenzi wa kituo cha afya, kituo cha polisi na uwekaji wa taa za barabarani ni miradi muhimu ambayo wananchi walikuwa wakisubiri muda mrefu.


“Unajua wananchi wanahamamu ya kuona miradi ikitekeleezeka na wanahamu ya kuona ikikamilika kwa haraka zaidi naamini kila jambo tunaloingia mkataba leo litafanyika kwa haraka” amesema Nampanye

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI