Header Ads Widget

KIFO CHA MARIAM CHANZO NI WAHUDUMU WA AFYA SIO KUKOSA FEDHA

 

Tume iliyoundwa na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu kuchunguza kifo Cha mjamzito, Mariam Zahoro imebaini kuwa kifo hicho kilitokana na uzembe wa wataalam wa Afya na sio sababu ya kukosa fedha za kugharamia matibabu yake kiasi cha Tsh: 150,000.


Waziri Ummy amesema hayo Novemba 27,2023 baada ya kupokea taarifa kutoka kwa tume ya Uchunguzi aliyoiunda ikiongozwa na Dkt. Ally Said ambae ni Daktari bingwa na Mhandiri wa Magonjwa ya Akina Mama na Uzazi kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).

 

“Kifo cha Mariam Zahoro kilitokea tarehe 11 Novemba, 2023 katika kituo cha Afya cha Kabuku baada ya kushindwa kujifungua kwa njia ya kawaida na hivyo kuhitaji kufanyiwa huduma ya dharura ya upasuaji ambapo huduma hiyo hakupatiwa kwa wakati na hivyo kupelekea kupoteza maisha.” Amesema Waziri Ummy


Amesema, kifo hicho kimetokea kwa sababu ya Mtaalamu wa huduma ya Usingizi na ganzi kutopatikana licha ya kupigiwa simu mara kadhaa kuwa kuna dharura pamoja na Daktari wa zamu namba 2 kuchelewa kufika licha ya kupigiwa simu mara nyingi kuwa kuna dharura. 


“Daktari huyo namba 2 hata alipofika hakuchukua hatua za kuokoa maisha ya mgonjwa kama kumpa rufaa baada ya mtaalamu wa usingizi kutopatikana au kutuma mtu wa kwenda kumgongea mtaalam wa huduma za usingizi.” Amesema Waziri Ummy 


Aidha, Waziri Ummy amesema Nchi yetu inaongozwa na Sheria na taratibu hivyo amelitaka Baraza la Madaktari Tanzania pamoja na Baraza la Wauguzi ambao wamepelekewa taarifa za Madaktari hao kuharakisha Mchakato wa Kusikiliza mashauri baada ya kukamilika kwa muda wa siku 14 baada ya wao kujieleza huku akisisitiza watumishi hao kutorudi kazini. 


Pia, Waziri Ummy amepiga Marufuku kwa Viongozi na wataalamu kufanya maamuzi ya kuwatoza fedha wananchi kupitia vikao vya makubaliano pasi na kuwashirikisha wananchi kutokana na Majibu ya taarifa ya Uchunguzi kuonyesha kuwa yaliweka makubaliano ya kuwatoza wajawazito gharama hizo za Shilingi laki na nusu kwa watakojifungua kwa Upasuaji.


Wakati akisoma taarifa hiyo Mwenyekiti wa Tume ya uchunguzi Dkt Ali Said ambaye ni Daktari Bingwa na Mhandiri wa  Magonjwa ya Akina Mama na Uzazi kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) amesema walifanya mahojiano na watumishi nane na sita kati yao walihusika kumhudumia Marehemu Mariamu.


Amesema, Daktari wa upasuaji aliyekuja kwa kuchelewa akilaumiwa kushindwa kumpa rufaa mjamzito huyo baada ya kumkosa mtaalamu wa sindano ya usingizi au kuchukua hatua ya kwenda kumgongea kwakua hakuwa akiishi mbali na kituo cha Afya kilipo. 


Marehemu MARIAM ZAHORO alikua na Umri wa miaka 39 ikiwa ni mimba yake ya tano iliyomsababishia umauti

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI