Header Ads Widget

ZAIDI YA MIRADI 1,400 YENYE THAMANI YA TRILIONI 5.3 YAZINDULIWA WAKATI WA HITIMISHO LA MWENGE.

 


Na: FRANCO NKYANDWALE.  MANYARA MATUKIO DAIMA APP.

Zaidi ya miradi 1400 yenye thamani ya shilingi Trilioni 5.3 imezinduliwa wakati wa hitimisho la mwenge wa uhuru lililofanyika leo Mkoani Manyara.

Taarifa hiyo imetolewa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt, Samia Suluhu Hassan ambapo Miradi 1,424 ilipitiwa kwa nyakati tofauti kuhitimishwa katika Kilele Cha Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2023 Mkoani Manyara.


Sherehe za kuhitimisha mbio hizo zimefanyika Uwanja wa Tanzanite Kwaraa na zimeenda sambamba na Kumbukumbu ya Miaka 24 ya kifo Cha Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, leo Oktoba 14.


Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2023 umekimbizwa kwa Siku 196 kwenye Mikoa 31 na Halmashauri 195 chini ya Vijana 6 kwenye km 27,437.


 Miradi 1,424 iliyopitiwa kati hiyo Miradi 7 yenye thamani ya Shilingi Bil.7.9 ilikataliwa kutokana na kugubikwa na dosari.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI