Header Ads Widget

WALIMU WA HISABATI WATAKIWA KUTUMIA MBINU SHIRIKISHI

 


WALIMU wa somo la Hisabati Wilayani Kisarawe Mkoani Pwani wametakiwa kutumia mbinu shirikishi za ufundishaji na ujifunzaji wa somo hilo ili kuleta matokeo chanya kwa wanafunzi.


Hayo yalisemwa Wilayani Kisarawe na Ofisa Elimu Mkoa wa Pwani Sara Mlaki wakati wa kufunga mafunzo ya kusimamia na kutekeleza mtaala wa somo la hisabati elimu ya msingi kwa walimu wa somo hilo.


Mlaki alisema kuwa mafunzo hayo yawe chachu ya kuboresha ufundishaji na ujifunzaji wa somo la hisabati ili kuinua ufaulu katika Halmashauri ya Kisarawe na mkoa mzima kwa jumla.


Kwa upande wake mwezeshaji kitaifa wa somo la hisabati kupitia Shule Bora Emanuel Mwanja alisema kuwa walimu wanapaswa kufundisha kutumia zana za hisabati na mahiri husika na zinazoendana na maisha ya kila siku.


Naye Ofisa mthibiti ubora wa shule Wilaya ya Kisarawe Mbwelu Mwankina ambaye ni mtaalamu wa hisabati alisema kuwa wamebuni mkoba wa kanuni za somo la hisabati kuanzia darasa la tatu hadi la saba.


Mafunzo ya walimu kazini yanahusu moduli ya hisabati iliyoboreshwa kulingana na rasimu ya mtaala mpya wa elimu ya msingi yameandaliwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania yaliandaliwa kwa kushirikiana na programu ya Shule Bora kupitia ufadhili wa serikali ya Uingereza (UKAID).

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI