Na fatma Ally, Matukio DaimaApp, Dar
Wafanyabiashara na wamiliki wa kampuni wametakiwa kusajili majina ya biashara zao brela ili kuweza kuwekea ulinzi ambao utawapa umiliki halali wa biashara zao.
Rai hiyo imetolewa ma Afisa leseni kutoka brela Ndeyanka Mbowe wakati alipokuwa katika Kilele cha maonesho ya viwanda ambayo yameandaliwa na Shirikisho la Viwanda CTI pamoja na Wakala wa Serikali anayehusika na usajili wa biashara pamoja na majina ya kampuni Brela.
Amesema kuwa, maonesho yamefanyika kwa mara ya kwanza ambapo muitikio umekua mkubwa sana wa watu kutembelea katika maonesho hayo ambapo ameitaka Tantrade na Cti mwakani kuoneza ubunifu zaidi ili watu wengi waweze kushiriki na kuweza kutangaza biashara zao.
Ameongeza kuwa, kwa Brela ni mdau mkubwa sana kwenye maonesho hayo ya viwanda, ambapo amekwenda brela kukutana na wadau wake, kwani watu wanapoanzisha viwanda nchini ni lazima kwanza wasajili viwanda vyao brela na kupata leseni ya biashara kutoka brela.
"Muitikio wa watu kuja kwenye maonesho haya ni mkubwa sana wamekuja kwa wingi kutaka huduma zetu ikiwemo kusajili biashara, wengi wao walitaka kuja kufahamu namna ya kusajili majina ya biashara na kwenye makampuni na mambo mengine "amesema Ndeyanka.
Hata hivyo, Cti na Tantrade wanatakiwa kuwa wabunifu zaidi kwani maonesho haya ni chachu ya kutoa fursa kwa wafanyabiashara kuweza kutangaza bidhaa zao na kukuza sekta ya viwanda na kupata fursa mbalimbali kwani wanakutanishwa na watu kubadilishana nao uzoefu.
0 Comments