Header Ads Widget

NAIBU WAZIRI MKUU DKT BITEKO ATOA POLE KWA MWANAMICHEZO WA SHIMIWI ALIYEFARIKI IRINGA






NAIBU waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Dotto Biteko ametoa pole  kwa wanamichezo wa SHIMIWI kufuatia Kifo cha mwanamichezo  Hamisi Ally aliyefariki wakati wa mashindano  hayo mkoani Iringa .


DKT Biteko ametoa pole hiyo Leo  katika viwanja vya Samora wakati akifungua mashindano  hayo ya SHIMIWI kitaifa mkoa wa Iringa .

Alisema Kifo cha mwanamichezo huyo ni pigo Kubwa kwa wanamichezo pamoja na familia yake .

Akizungumzia michezo  hiyo ya 37 ya SHIMIWI  waziri Dkt Biteko alisema michezo hiyo ni muhimu sana kwa watumishi wa umma na kuwa michezo hiyo itaendelea kuboreshwa mwaka hadi Mwaka na SHIMIWI wasikubali Siasa uchwara kuvuruga michezo hiyo .

Alisema shabaha ya michezo hiyo ni Kubwa kwa maana ya kuimarisha afya Njema kwa watumishi na watakwenda kuonesha tija sehemu ya kazi .


Waziri Dkt Biteko ambae alimwakilisha Rais Dr Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi huo alisema Serikali imepiga hatua Kubwa katika Sekta ya michezo na Serikali imekusudia kuongeza tija ya michezo kwa watumishi wa umma .

Alisema sera ya michezo nchini ni kielelezo tosha cha kuimarisha utamaduni wa mtanzania na hivyo Serikali itaendelea Kuunga Mkono jitihada zote za michezo .

Hivyo alitaka Wizara na idara zote za Serikali kuendelea kuimarisha michezo mahali pa kazi Ili kuendelea kuboresha zaidi Sekta ya michezo ikiwa ni pamoja kutumia michezo kukemea vitendo vya Rushwa na upotevu wa fedha za Miradi katika idara zao .

Pia alisema kupitia michezo hiyo pia kuendeleza mapambano mbali mbali kama vita dhidi ya UKIMWI na mapambano mengine .

Katika kuendeleza michezo nchini aliagiza Kila taasisi kutenga viwanja vya michezo Ili kuendeleza michezo mahali pa kazi .

Aidha alitaka watumishi na wanamichezo kuendelea kutangaza nchi kupitia Sekta ya Utalii pamoja na kuendelea na mapambano dhidi ya uharibifu wa Mazingira Ili kuondokana na mabadiliko ya Tabia Nchi .

Pia waziri Dkt Biteko alitaka michezo hiyo kuimarishwa pia mashuleni Ili kujenga Sekta ya michezo nchini .


Katika hatua nyingine waziri Dkt Biteko alionya watumishi wa umma kuacha kuchukulia michezo hiyo kimazoea kwa kukwepa kushiriki michezo hiyo na kutaka viongozi wote mwakani kuhakikisha wanashiriki michezo pamoja na kuwawezesha kikamilifu washiriki wa michezo.

"Natamani kuona washiriki wa michezo hii wanawezeshwa kikamilifu Ili kuondokana na unyonge kama ni Watu ambao wamepewa lifti katika mashindano hayo "
















Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI