Header Ads Widget

MAKALLA:TUNAOMBA OFISI YA MTAKWIMU MUWAPE VIJANA WETU MAFUNZO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI BILA KUJALI ITIKADI YA VYAMA.

CHAUSIKU SAID,MATUKIO DAIMAAPP MWANZA.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Amos Makalla ameiomba ofisi ya mtakwimu wa serikali kuangalia idadi na umri wa vijana walioko mkoani hapa kuhakikisha wanawapa elimu ya sensa ya watu na makazi bila kujali taasisi wanazotokea na itikadi ya vyama vyao.


Hayo ameyabainisha leo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya matumizi ya matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 Kwa viongozi, watendaji wa Mkoa,kamati ya sensa pamoja na wawakilishi wa makundi mbalimbali.

Makalla amesema kuwa ni muhimu kukutana na makundi hayo ya vijana na kuwaeleza wao ndio nguvu kazi ya Taifa Kwa kufanya shughuli za kiuchumi na sio kushika jembe pekee.

"Mkawape semina vijana ya matokeo ya sensa ya watu na makazi na kueleza wao ndio nguvu kazi ya Taifa na takwimu zinadhibitisha" Alisema Makalla.


Kwa upande mwingine ameeleza kuwa kuwa takwimu za sensa ya watu na kazi zitasaidia kutatua migogoro mbalimbali ya mvutano ya vijiji, mitaa pamoja na kutambua sehemu inayopaswa kupelekewa maendeleo.


"Hivi sasa tumepata matokeo ya sensa yatatusaidia kupanga mipango na kufahamu idadi ya watu na kuonesha wapi idadi kubwa ya watu palipo pamoja na kutatua migogoro ya wanasisa wanaoshinikiza Miradi ipelekwe katika maeneo ambayo yana watu wachache na kuacha maeneo yenye idadi ya watu wengi" Alisema Makalla.

Meneja idara shughuli za takwimu Taifa Benedict Mugambi amesema kuwa wanatumia matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 kwa kuwaelimisha Watanzania wote kuanzia ngazi ya Mkoa Hadi mpaka kijiji.


Mugambi ameeleza kuwa mafunzo hayo Msingi wake ni wananchi wapate elimu baada ya sensa ya watu na makazi kufanyika ili waweze kufahamu matumizi sahihi ya takwimu hizo zinawezaje kuwasidia kwenye mipango yao mbalimbali.


"Tumeona kabsa katika baadhi ya maeneo ambayo tumepita kufanya mafunzo watu hufanya utashi wao binafsi kupeleka maendeleo Kwa sababu ni kiongozi na jambo Hilo kuwa na athari kubwa sana" Alisema Mugambi.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI