Header Ads Widget

UONGOZI WA SHULE ZA LEGACY KUZISAIDIA SHULE ZA SERIKALI IRINGA

Na Simon Joshua - Matukio Daima App, Iringa.

Uongozi wa Shule za Legacy Academy mkoani iringa umeahidi kuzisaidia shule za serikali mkoani humo zinazokabiliwa na changamoto mbalimbali za wanafunzi ili kuwasaidia watoto hao kufikia ndoto zao bila vikwazo vinavyoweza kuepukika.


Maneno hayo yametolewa na mwakilishi wa Shule za Legacy Academy Mwl. Joachim Mapunda alipokuwa akizungumza na watoto, wazazi na walimu wa Shule ya Msingi Mkimbizi kama mgeni rasmi katika mahafali ya kuwaaga wanafunzi wa darasa la saba shuleni hapo yaliyofanyika hapo jana Tar 21/09/2023.


Mapunda anasema yeye kama mwakilishi wa Legacy Academy Schools ameguswa na maisha wanayoishi watoto wa shule za serikali hivyo Legacy Academy itasaidia kujenga uwanja wa mpira na jiko kwa ajili ya kupikia chakula cha watoto ili wasishinde njaa wakiwa shuleni.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS