Na Mwandishi wetu, Mtwara
Wananchi 203 walioharibiwa mazao wakati wa utafutaji wa gesi asilia katika eneo la ntorya katika kijijiji cha nanguruwe mkoani mtwara wameiopongeza TPDC kwakuchukua hatua hiyo.
Akizungumza Amina Mchira mkazi wa Likonde alisema kuwa amefurahi sana kupata malipo hayo ambayo amesubiri kwa muda mrefu ambapo ni wananchi 203 wanaotarajia kulipwa zaiid ya sh65 milioni.
“Yaani nimefurahi kupata hii fidia hii nilikuwa naumwa kwa muda mrefu lakini hatimae nimepata malipo yangu ambayo naamini kuwa yatanisaidia pamoja na familia yangu maisha yamekuwa magumu lakini hiki kidogo kitakuwa msaada mkubwa zaiidi” alisema Mchira
Ernest Joseph Mkazi Likonde alisema kuwa anaishukuru serikali kwakusimamia haki ya wananchi hao ambao wamepisha mradi huo muhimu kwa taifa.
“Tunafahamu umuhimu wa kuwa na uwekezaji wa miundombinu ya gesi ambayo imekuwa ikisaidia nchi kwa muda mrefu ikiwemo kuzalisha umeme kutumika viwandani na pia”
Mjiologia kutoka TPDC Patrick Kabwe alisema kuwa malipo yameshafanywa kwa awamu tatu ambapo sasa ni ya nne ambayo inatokana na wananchi ambao hawakuwa na akaunti.
“Katika awamu hii tunalipa wananchi 203 tu kutokana na changamoto mbalimbali ambapo zaiid ya milioni 65 kuweza kuwalipa kwasasa tuko katika maandalizi ya kuchimba gesi katika kisima cha chikumbi 1 ambapo tutachimba 2024 ambapo ntolya1-2 zote zimeshachimbwa na kugunduliwa kuwa na gesi futi za ujazo bil1.6”
Jacobo Haule kutoka kitengo cha mawasiliano TPDC alisema kuwa wamekuja kamilisha malipo ya fidia kwakushirikiana na mwekezaji wa kampuni ya ARA petroleum ambapo tafiit zinaendelea.
“kwa mujibu wa sheria ya nchi inatutaka kulipa fidia ambayo ni awamu ya nne tutalipa kwa siku 10 ambapo tumeshaliza zaidi ya sh1 bil ambapo wananchi hawa 203 ndio tunaenda kuwalipa sasa”
Nae Mwakilishi wa kampuni ya ARA Judith Kalugasha alisema kuwa malipo hayo yalichelewa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kufariki lakini wenigne kushindwa kuwa na akaunti za benki.
0 Comments