Elizabeth Ntambala Katavi
MAREHEMU Philip Method Mtepa,Mwenyekiti wa Chama Cha Mpindunzi (CCM) Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi ameagwa leo katika makazi yake yaliyopo mtaa wa Airtel Manispaa ya Mpanda ambapo leo atasafirishwa kwenda kuzikwa mkoani Rukwa.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Katavi,Iddy Kimatta amesema kuwa kuna pengo kubwa limeachwa na marehemu kutokana na muda mrefu amekitumikia chama kwa uzalendo mkubwa.
Uzalendo kwa Chama na Taifa wa aliyekuwa mwenyekiti huyo sio wa kutiliwa shaka hata kidogo ambapo vijana wanamambo mengi ya kujifunza kutoka kwake.
Kimata amasema kuwa Marehemu ni moja ya viongozi ambao walichaguliwa kwenye uchanguzi wa ndani ya chama mwaka 2022 ambapo kwa pamoja walikuwa wamejiwekea malengo makubwa ya kiutendaji yatakayo hakikisha chama kinapiga hatua kubwa ya kuisimamia serikali pamoja ustawi wa chama kiujumla.







0 Comments