Na MWANDISHI WETU,ZANZIBAR
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha ACT- Wazalendo Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, amewataka Viongozi wa Matawi wa Chama hicho waliochaguliwa kwenye uchaguzi wa ndani wa hivi kuelewa kwamba wao ndio msingi muhimu unaobeba dhima ya kuwapata viongozi bora katika ngazi za majimbo, wilaya na mikoa wenye uwezo wa kusaidia kujenga chama na kupata ufanisi mkubwa ili kutimiza malengo ya chama hicho yaliyowekwa.
Mhe. Othman ameyasema hayo huko ukumbi wa Majid Kiembesamaki Wilaya ya Magharib Unguja, alipozungunza na viongozi mikoa, ngome za wanawake na wazee, pamoja na Viongozi wapya wa Matawi ya chama hicho kutoka Mikoa yote ya Unguja Kichama, kufuatia kukamilika uchaguzi wa Viongozi wa matawi hivi karibuni.
Mhe. Othman ambaye pia ni makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar , amefahamisha kwamba kuwepo kwa viongozi hao makini pia ndio msingi madhubuti katika kujenga na kuimarisha chama hicho ambao watasaidia kuendeleza jitihada za kufanikisha maelngo na dhamira ya chama hicho ya kuwepo Zanzibar yenye umoja na mshikamano wa kuiletea maendeleo Zanzibar.
Amefahamnisha kwamba chama hicho kinahitaji viongozi makini watakosaidia jitihada za chama hicho ya kuwepo Zanzibar moja na kuwataka kwenda kufanyakazi za kutumikia chama kwa juhudi kuwa katika kutimiza maono ya chama hicho kwa kuzingatia uzalendo wa kuipoenda nchi yao.
Aidha amewataka viongozi hao waliochaguliwa kujenga mashirikio makubwa na uongozi wa ngome zote za chama hicho ili kuweza kujenga taasisi imara itakayowezesha kukipatia ushindi chama hichi katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2025.
Mhe. Othman amesema kwamba kufanyika kwa chaguzi hizo katika misimingi ya kidemokrasia ni kelelezo muhimu kinaochonesha kwamba hakuna walikwenda kupanga safu kwa kuwabeba baadhi ya wagombea lakini ni wale waliofahamu wajibu na dhamira ya chama hicho ya kuijenga Zanzibar mpya.
Makamu mwenyekiti huyo amewapongeza viongozi walichanguliwa na kuwataka kutokulala na badala yake wafanye kazi kubwa ya kukitumikia chama sambamba na kuwashukuru wagombea walioshindwa kwa kuonesha ukomavu na kwamba kushindwa kwao hakuoneshi kwamba ni dhaifu kwa kuwa chama hicho kinahazi kubwa ya viongozi wengi wazuri katika kusimamia safu mbali mbali.
Naye Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho Zanzibar ambaye pia ni waziri wa Afya Afya Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui amewataka vijana wa chama hicho kutorudi juma na badala yake waendeleze umoja na msihakamano jutakaosaidia kupatikana mafanikio ya chama na Zanzibar kwa jumla.
Kwa upande wake Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho Ismail Jussa Ladhu amewataka vijana kuelewa kwamba wao ni tegemeo kubwa la maendeleo na umoja wa Zanzibar na kwamba kuna haja ya kujifunza na kuelewa masuala mbali mbali yanayohusu historia ya Zanzibar katika kusaidia ujenzi wan chi yao.
Mapema Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Chama hicho Said Rashid Muhene amesema kwamba kazi ya uchaguzi wa viongozi ngazi yay a matawi ya chama hicho unguja na Pemba imefanyika kwa ufanisi mkubwa na kwanga hivi karibuni utaendelea katika kuwapata vuiongozi wapya wa ngazi ya majimbo.
0 Comments