Header Ads Widget

KONGOLE NIC KWA KUMUDU USHINDANI LICHA YA KUWEPO MAKAMPUNI MENGINE


SHIRIKA la Bima la Taifa (NIC) linajivunia kumudu ushindani licha ya kuwepo na Makampuni zaidi ya thelathini kwenye soko la Bima Tanzania, imeweza kumudu ushindani kwa kufanya vizuri baada ya Shirika hilo kufanya maboresho tangu mwaka 2019.


Kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya Bima Shirika limeendelea  kutoa elimu ya Bima kwa wananchi kupitia vyombo mbalimbali vya Habari, ikiwemo Radio, Runinga, Magazeti, Machapisho pamoja na makongamano ili watanzania wengi wajiunge na huduma za Bima.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo la Bima la Taifa, Dkt. Elirehema J. Doriye, alipokuwa akizungumza na Wanahabari Jijini Dar es salaam katika mwendelezo wa mikutano ya Taasisi za Umma na Vyombo vya Habari unaoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina.



Eidha Dkt. Elirehema amefafanua kuwa Kutokana na ukuaji wa Shirika la Bima la Taifa katika nyanja mbalimbali ikiwemo mwendelezo mzuri wa kupata faida na ukuaji wa mtaji, NIC  limeendelea kuvutia wateja wa bima kwa vigezo vifuatavyo: Uzoefu, Hekima na Urithi, Thamani, Ubora na Imani, Kuwa na vigezo vya kimataifa vya utoaji wa huduma bora kwa wateja.


"Ongezeko la mitaji Katika kukabiliana na uwezo mdogo wa kuhimili hasara inayoweza kutokea (low underwriting capacity) tumefanikiwa kuongeza mtaji  wa kiasi cha Shilingi bilioni 12.05 mwezi Aprili, 2022 sawa na ongezeko la asilimia 408.47 kutoka mtaji uliokuwepo wa kiasi cha Shilingi bilioni 2.95 na kufikia mtaji wa kiasi cha Shilingi bilioni 15 kilichopo sasa."amesema na kuongeza kuwa


"Utoaji wa gawio, Kwa mwaka ulioishia Juni, 2022 tumetoa gawio la Shilingi bilioni 2.0 kwa Serikali ikilinganishwa na gawio la kiasi cha Shilingi bilioni 1.5 lililotolewa mwaka ulioishia Juni 2021.



"Ukuaji wa Uwekezaji katika hati fungani za Serikali kwa mwaka 2021/22 umefikia kiasi cha Shilingi bilioni 105.64 uKIlinganisha na kiasi cha Shilingi bilioni 51.58 kilichokuwepo mwaka 2019/20. Ongezeko hili ni sawa na wastani wa asilimia 52.40 kwa mwaka. Uwekezaji katika amana za Benki mwaka 2021/22 umefikia kiasi cha Shilingi bilioni 32.23 ukilinganisha na Shilingi bilioni 19.53 kilichokuwepo mwaka 2019/20. Ongezeko hili la uwekezaji kwenye amana za Benki ni sawa na wastani wa asilimia 32.54 kwa mwaka.



" Pia Ukuaji wa mtaji kwa wanahisa Ufanisi katika uendeshaji, umewezesha ukuaji wa Mtaji wa wanahisa kuongezeka kutoka Shilingi bilioni 72.16 mwaka 2019/20 hadi Shilingi bilioni 217.07 mwaka 2021/22. Ukuaji huu wa mtaji ni sawa na ongezeko la wastani wa asilimia 100.40 kwa mwaka."amesema.


Katika hatua nyingine amesema "Mali za NIC, zimekua kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo, kutoka mali zenye thamani ya Shilingi bilioni 350.36 mwaka 2019/20 hadi kufikia mali zenye thamani ya Shilingi bilioni 423.99 mwaka  2022. Ukuaji huu ni sawa na ongezeko la wastani wa asilimia 10.51 kwa mwaka.


"Faida ghafi imeongezeka kutoka Shilingi bilioni 33.65 mwaka 2019/20 hadi Shilingi bilioni 63.21 mwaka 2021/22 sawa na asilimia 43.91 kwa mwaka. Aidha, kutokana na faida mfululizo tumeweza kupata malimbikizo ya faida ya Shilingi bilioni 45.74 kufikia Juni, 2022 kutoka kiasi cha malimbikizo ya hasara ya shilingi bilioni 19.31."amesema


"Tumeweza kulipa kodi ya mapato Serikalini kutokana na faida inayopatinana ambapo ulipaji huo umeongezeka kutoka Shilingi billioni 11.86 mwaka 2019/20 hadi Shilingi bilioni 15.14 mwaka 2021/22 sawa na wastani wa asilimia 13.80 kwa mwaka.


"Katika kipindi cha miaka mitatu tumelipa madai ya bima za wateja ambapo hadi kufikia Juni 2022, tumelipa jumla ya Shilingi bilioni 33.79 kwa bima za Maisha na Shilingi bilioni 40.18 kwa bima za mali na ajali.


"Usimamizi madhubuti wa matumizi pamoja na kutoa mafunzo kwa watumishi kumeongeza ufanisi na kuondoa matumizi yasiyo na tija jambo lililoshusha gharama za uendeshaji na kuongeza faida."amesema na kufafanua kuwa


"Kutokana na kuchukua hatua nilizozitaja hapo juu tuweza kuondoa hasara kwa kuongeza mapato kutoka Sh. bilioni 76.45 2019/20 hadi Sh. bilioni 103.94 2021/22. Ongezeko hili ni sawa na asilimia 17.98 kwa mwaka."amesema Dkt. Elirehema.


Mabadiliko ya Utendaji NIC Insurance imekuwa ikitekeleza shughuli zake kwa kuzingatia mwongozo wa uanzishwaji wake (“MEMART”) na Sheria ya Bima Na. 10 ya mwaka 2009.


NIC insurance ilianza kuchukua hatua za mabadiliko ya kiutendaji ili kujiimarisha kibiashara tangu Julai 2019.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI