Na Simon Joshua - Matukio Daima App, Iringa.
Askari wa jeshi la Polisi mjini Iringa wametakiwa kuwa na ujuzi wa Kompyuta na Udereva ili viwasaidie katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku wawapo kazini au wawapo nyumbani.
Hayo yamesemwa na Kamishna wa jeshi la Polisi mjini Iringa, Kamanda Alan Bukumbi alipokuwa akizindua mafunzo ya utayari kazini katika kambi ya Askari wa kutuliza ghasia (FFU) mjini Iringa.
Katika uzinduzi huo, Kamanda Bukumbi amewataka Askari hao kudumisha nidhamu na utii kwa viongozi wao na Askari wenzao ili kuleta ufanisi wa kazi zao.
0 Comments