Header Ads Widget

CHUO CHA TAIFA CHA USAFIRISHAJI NIT KUWA NA MPANGO WA KUANZISHA USAFIRI WA CABLE CAR

 

Chuo cha Taifa Cha  usafirishaji ( NIT)kimekusudia kujikita katika mafunzo ya matumizi ya magari maalumu yanayotumia nyaya za umeme (Cable Car)ili kurahisisha usafirishaji katika maeneo yenye Changamoto ya Usafiri.


Hayo yameelezwa na Naibu  Mkuu wa chuo hicho Zainab  Mshana wakati akiwa katika mafunzo ya maafisa usafirishaji na madereva wakuu Yaliyofanyika Mkoani Kilimanjaro.


Aidha amesema kuwa kutokana kutokuwepo kwa changamoto ya Usafiri hapa nchini katika maeneo mengi Bado Kuna maeneo ambayo yanahitaji matumizi ya usafiri huo.


"Ninachoweza kusema ni kwamba malengo yetu ya kuendesha Mafunzo yalivyotolewa kwenye Sheria iliyoanzisha chuo ni kutoa mafunzo kwenye nyanja zote za usafirishaji lakini Kuna njia nyingine ya kutumia waya Cable"Alisema Zainab.

Sambamba na hayo ameendelea kusema kuwa njia hiyo imekuwa ikitumika katika nchi ambazo zimeendelea ambazo jiografia yake sio nzuri kimiundombinu kwa maana kwamba milima na mabonde kwa hiyo inabidi watumie hiyo njia ya (Cable Car) kama njia ya usafirishaji.


"Kwetu huku haijawa shida sana lakini nimesema ni jicho lingine la kitafiti watu wanaweza wakaangali ,nimetaja  Tanapa pale wapi ni vyema wakaangalia namna ya kuboresha utalii pia "Alisema Zainab.


Akifungua Mafunzo hayo Mkuu wilaya ya Moshi Kisare Makori amesema kuwa  utoaji wa mafunzo hayo  yana umuhimu kwani yatawasaidia Madereva kupunguza changamoto wanazokumbana nazo.

Amesema kuwa mara baada ya mafunzo hayo watakuwa mabalozi wazuri wa chuo cha Taifa Cha usafirishaji kwa kuendesha na kwa kusimamia magari kwa uweledi mkubwa na kusaidia kupunguza gharama za uendeshaji  katika Taasisi wanazotoka.


"Natoa wito kwa uongozi wa chuo kuendelea kuwa wabunifu na kufanya kazi kwa uweledi mkubwa ili kukifanya chuo kuwa mahali sahihi pa kupatia mafunzo stahiki kama ambavyo mnayafanya" Alisema Makori.


Nao madereva walioshiriki katika mafunzo  akiwemo Joris Moris ambaye ni afisa usafirishaji wilaya ya karatu amesema kuwa   Mafunzo  hayo yatawasaidia kuboresha utendaji wa kazi zao .


"Kwa Mimi mafunzo haya yataenda kuwa Bora kwangu katika kuboresha majukumu yangu ikiwa ni madereva ninao waongoza pamoja na magari yote ninayosimamia katika Halmashauri yangu"Alisema.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI