Header Ads Widget

MAKATIBU KATA WATAKUWA KUZITUMIA PIKIPIKI WALIZOPEWA KUKIJENGA CHAMA.


Na Chausiku Said-Matukio Daima App, Mwanza.

Makatibu kata wa chama Cha mapinduzi CCM Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza wametakiwa kutumia pikipiki walizopewa katika kukijenga na kukiimarisha chama hicho na sio kutumia katika shughuli zao binafsi.


Hayo yamebainishwa na Katibu wa Wilaya hiyo Hassan Miranga wakati akikabidhi pikipiki 19 Kwa makatibu kata zilizotolewa na Mbunge Angelina Mabula kupitia The Angelina Foundation na kueleza kuwa hawataraji kuona katibu yeyote anatumia pikipiki hizo kinyume na katiba.

Miranga ameeleza kuwa mujibu wa kanuni na taratibu za chama hicho pikipiki hizo zinatakiwa kwenda kufanya kazi za chama na sio matumizi mengine.


"Kulikuwa na tatizo la usafiri sasa umapatikana tuna matarajio  mnaenda kukiimarisha na kukijenga chama Kwa uweledi" Alisema Miranga.


Ameeleza kuwa katibu yeyote atakaye kiuka maelekezo ya katiba na kanuni ya chama Cha mapinduzi, chama hakitasta kumchukukia hatua Kwa kumnyang'anya pikipiki.

Katibu wa Mbunge Charles David akizungumza Kwa niamba ya Mbunge ameeleza kuwa lengo na  matarajio ya kukabidhi pikipiki hizo ni kurahisisha usafiri Kwa makatibu hao wakati wanatekeleza majukumu ya kazi 


"Tumeona kumekuwepo na changamoto mbalimbali Kwa makatibu pale wanapohitajika kwenye vikao na shughuli mbalimbali za chama kwenye matawi na Mitaa yao" Alisema David.


Aidha ameeleza kuwa jukumu kubwa walilobaki nalo makatibu hao ni kuhakikisha wanasimamia na kukisemea na kuinadi ilani ya chama.

Baadhi ya makatibu waliopata pikipiki hizo wameeleza kuwa watazitumia kuhakikisha wanakijenga chama na jumuiya zake Kwa kufanya kazi zote kw a uweledi.


"Makatibu ndio walezi wa jumuiya za chama kwenye kata husika tulikuwa na ratiba za kufanya vikao kwenye mashina lakini tulipata  changamoto ya kufika kwenye vikao hivyo Kwa sasa mbunge ameturahisishia kufika Kwa urahisi".

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI