Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP DODOMA
MKURUNGEZI Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Profesa Mohamed Janabi amesema kuwa wako mbioni kuanza kutoa huduma za upandikizaji mimba kwa mashine maalum (IVF - In vitro Fertilization).
Prof Janabi ameyasema hayo leo jijini hapa alipokuwa akizungumza na wanahabari Jijini Dodoma kuhusu utekelezaji wa shughuli za Hospitali ya Taifa Muhimbili na mwelekeo wa mwaka 2023/24
"Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan imekamilisha ununuzi wa mashine za kusaidia upandikizaji mimba zilizogharimu Shilingi Bilioni 1,"Amesema Prof Janabi.
Aidha ameeleza kuwa huduma za upandikizaji mimba zitaanza kutolewa hivi karibuni Mara baada ya kukamilisha usimikaji wa mitambo.
"Tatizo la watu kutopata ujauzito ni kubwa na Watanzania wengi wamekuwa wakitoka nje ya nchi kupata huduma za kupandikizwa mimba kwa gharama kubwa hivyo Serikali imesogeza huduma hizo karibu hivyo zitaanza kupatikana hapa hapa nchini," Amesema .
Na kuongeza"Jengo lishakamilika na Muhimbili tulitenga chumba cha kutolea huduma hizo na kwasasa tunasubiri usimikaji wa mitambo hiyo ikamilike ndo tuanze kutoa huduma hizo, na wananchi wanaohitaji huduma hizo hawata kwenda nje ya nchi kupata huduma hizo”, ameeleza Prof. Janabi.
Prof. Janabi amesema kuwa Hospitali tayari ina wataalamu waliowezeshwa na mafunzo ya utoaji wa huduma hiyo na wamesharejea kutoka masomoni hivyo kusubiri kuanza kwa kutolewa kwa huduma hizo.
Hata hivyo amesema kuwa watanza na kliniki za kawaida kisha hatua za upandikizaji zitafutwa kwa kushirikiana na wataalamu elekezi kutoka nje ya nchi ili kufanyikisha huduma za upandikizaji mimba ambao wataelendelea kuwajengea uwezo wataalam wa Hospitalini.
0 Comments