Na Gift Mongi MATUKIODAIMA APP MOSHI
Ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya serikali kupitia waziri wa viwanda na biashara Dkt Ashantu Kijaji wakala wa usajili wa biashara na Leseni (BRELA) imewataka wafanyabiashara wa mazao ya Kilimo nje ya nchi kurasimisha biashara zao ili kuweza kuondoa vikwazo vilivyokuwa vikiwakabili hapo mwanzo.
Hata hivyo kurasismishwa Kwa biashara hizo mbali na kuondoa vikwazo hivyo bali itawezesha kulindwa kwa biashara zao na kuachana na kufanya biashara kimazoea
Isdor Nkindi ambaye ni mkurugenzi wa usajili wa majina ya baiashara na makampuni kutoka BRELA anatoa rai hiyo wakati wa utoaji wa mafunzo kwa wauzaji wa mazao ya kilimo nje ya nchi, mkoa wa Kilimanjaro.
'Tukirasimisha biashara zetu hizi tunaenda kufanya kazi bila woga au kuwa na misuguano isiyokuwa na ulazima hivyo nitoeni rai kwa wafanyabiashara kuchangamkia malengo haya mazuri ya serikali kwa kuwa yana lengo jema'anasema
Kwa mujibu wa Nkindi ni kuwa hivi karibuni serikali ilitoa maelekezo ya uzaji wa mazao ya kilimo nje ya nchi na kueleza kuwa haijakataza mtu yeyote kufanya biashara ya mazao hayo nje, ila kinachohitajika ni kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo iliyopo ikiwemo kurasimisha biashara.
'Yaani ipo hivi wafanyabiashara hawana uelewa na kuwa Wana tabia ya kupotoshana juu ya hizi sheria ikiwa ni pamoja na miongozo iliyowekwa na serikali ndio maana tumekuja hapa kutoa elimu'anasema
Shamsa Mwenegoha ambaye ni mfanyabiashara wa mazao ya nafaka katika eneo la Tarakea wilayani Rombo ambapo huuza nchi jirani ya Kenya amesema malumbano ya serikali na wafanyabiashara hao ndio yaliyopelekea kuzorota Kwa biashara hiyo kwani kila siku sheria zimekuwa zikibadilika bila ushirikishwaji.
'Tatizo serikali inafanya maamuzi bila kutushirikisha sisi kama wadau nadhani ipo haja sasa tukae katika meza ya mazungumzo kama sasa ili tuweze kufanya biashara bila bugudha
Judith Uronu aliiomba serikali kuona namna ya kuondoa urasimu na vikwazo vya kupeleka mazao nje nchi, ili kutoa fursa kwa wafanyabiashara kupata masoko ya nje.
Mwisho.
0 Comments