Agizo hilo limetolewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe John Makuri Imori katika zoezi la uzinduzi wa kitabu cha ufahamu wa kanisa halisi la mungu baba uliofanyika mkoani Hapa na kwamba viongozi wa dini wanapaswa kuendelea kuisaidia serikali kukabiliana na wahalifu kwa kueneza injili.
Akizindua kitabu hicho mgeni wa heshima Kissa Kasongwa mkuu wa wilaya ya Njombe amekiri kuwa kanisa Halisi limekuwa miongoni mwa makanisa yanayochochea amani katika wilaya na mkoa tofauti na makanisa mengine kwenye baadhi ya mataifa ambayo yamekuwa yakiripotiwa kujihusisha na makundi ya ugaidi.
Kiongozi mkuu wa kanisa hilo Baba Halisi amesema hivi sasa wameendelea kueneza injili kwa kutumia lugha ya kiswahili katika mataifa ya Rwanda,Uganda,DR Congo,Msumbiji na Kenya ambako pia wamekubaliwa kutokana na kazi njema ya kuhamasisha amani ambayo inawasaidia viongozi wa serikali kuwaongoza vyema wananchi.
0 Comments