Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Jumuiya ya umoja wa vijana UVCCM Mkoa wa Njombe imelaani vikali kauli zinazodaiwa kuwa na chembechembe ya ubaguzi zilizotolewa na Viongozi wa siasa, zinazoweza kuwagawa Watanzania.
UVCCM Njombe imefikia hatua hiyo kufuatia kauli zinazodaiwa kutolewa na viongozi wa siasa ambazo kwa namna moja ama nyingine zinaweza kuwagawa watu katika misingi ya ukabila, na utaifa.
Katika mkutano na waandishi wa habari mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Njombe Samuel Mgaya amesema kama umoja wa vijana haukubaliani na kauli hizo akitolea mfano wa kiongozi mmoja wa chama cha upinzani ambae hakumtaja waziwazi.
Amesema kitendo hicho kinaweza kuligawa taifa ambalo lina misingi ya Udugu,Umoja na mshikamano ambao uliasisiwa na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika harakati za kutafuta uhuru wa Tanganyika.
Aidha Mgaya amesema serikali ina dhamira njema ya kufanya uwekezaji wenye tija katika bandari zetu kutokana na kukua kwa teknolojia na hivyo Watanzania hawapaswi kubeza jitihada hizo za Rais Daktari Samia Suluhu Hassan.
Hata hivyo amesema kupitia uwekezaji huo Watanzania wengi watanufaika kwa ajira na Taifa litapata fedha nyingi zaidi ya linazopata sasa katika bandari zilizopo hususani ya Dar es salaam.
Wanasiasa mbalimbali wameendelea kujitokeza kupitia vyombo vya habari kupinga kauli zinazodaiwa kuwa ni za ubaguzi zilizotolewa na mwanasiasa huyo nguli wa upinzani kutokana na sakata la makubaliano ya kwenda kuendeleza bandari kupitia Kampuni ya DP W Ya nchini Dubai.
0 Comments