Na WILLIUM PAUL.
KATIKA kuhakikisha kuwa Askari Polisi kata wanafanya kazi katika mazingira mazuri na weledi mkubwa Serikali imeahidi kuhakikisha kila mahali wanapata vituo vya polisi pamoja na nyumba za kuishi polisi hao.
Hayo yamekuja baada ya Mbunge wa Jimbo la Moshi vijijini, Prof Patrick Ndakidemi kuhoji Bungeni Serikali imepeleka Askari Polisi kata katika kila kata nchini wenye renki ya Inspekta.
Aliendelea kuhoji kuwa, lakini polisi hao hawana makazi wala ofisi kwenye kata je Serikali wanampango gani wa kuwajengea Askari hao ofisi na nyumba za kuishi.
Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Khamis Hamza Khamis alisema kuwa, ni kweli wanatambua kwamba zipo ofisi zimechakaa kwa sababu ni za muda mrefu.
Naibu Waziri Hamza aliendelea kudai kuwa, pia wanatambua kuwa yapo maeneo mengine ofisi zinakuwa ni changamoto hivyo Serikali itajitahidi kuhakikisha kila mahali wanapata vituo vya polisi pamoja na nyumba za kuishi polisi kata hao.
Mwisho..
0 Comments