Header Ads Widget

RAIS SAMIA AWATAKA WAKULIMA NCHINI KUWEKA AKIBA YA CHAKULA

 



NA CHAUSIKU SAID_MATUKIO DAIMAAPP MWANZA 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan amewataka wakulima Nchini kuweka akiba ya chakula Cha kutosha ajili ya matumizi ya familia na kutouza nje.


Hayo ameyabaisha Leo katika uzinduzi wa tamasha la utamaduni Bulabo lililofanyika katika viwanja vya makubosho Bujora kata ya kisesa Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza ambapo tamasha Hilo hufanyika Kila mwaka baada ya mavuno.



Samia ameeleza kuwa Tanzania inapaswa kuwa na akiba ya chakula Cha kutosha kutokana  hesabu ya chakula kilichopo kwenye maghara ya serikali Tani 1 uhudumia watu 80 ambapo kiwango hicho haakitoshi.


" Tunapaswa kuwa na akiba ya kutosha ambapo  Tani moja tunaweza kuwahudumia watu 20 linapokuja swala uhaba wa chakula Tanzania iwe iko sawa na kuweka hakuna shida" Alisema Samia.


Ameeleza kuwa Ulimwengu mzima unatarajiwa kuwa na upungufu wa chakula hali itakayopelekea kuwepo Kwa mfumuko wa bei ya  chakula kutokana na athari za uvuko 19 vita vya urusi na Ukraine na mabadiliko ya hali ya hewa.



Moja ya dhima ya tamasha hili ni kumshukru Mungu Kwa ajili ya neema ya mavunomavuno kulima na kupanda ni swala moja lakini kupata kuvuna ni swala jinginejingine ni baraka na neema za Mwenyezi Mungu hususani katika zama hizi za mabadiliko ya tabianchi ambapo kilimo chetu kimeathiriwa na mabadiliko ya hali ya hewa.


"Sababu hizi tatu zimefanya Nchi yetu Kuwa kwa kipindi Cha miaka mitatu mfurulizo imefanya Nchi yetu haziwezi kuzalisha chakula Cha kutosha na kule kwenye chakula Kuna vita na vikwazo vya kutosha kiasi ambacho chakula hakiwezi kutoka kwenda sehemu yeyote ile" Alisema Dkt,Samia.




Mabadiliko ya tabianchi husababishwa na mafuriko pamoja na uwepo wa jua hali ambayo hupelekea upungufu wa chakula kuongezeka na kusababisha mfumko bei.


"Matarajio ya ulimwengu katika miaka hii ni  mfumko wa bei kuwa Asilimia 5% kutokana na kilichotokea mfumko wa bei Kwa sasa utaanzia Asilimia 10% Kwa mabara yote"Iwe bara la AsiaAsia, ulaya, marekani Afrika, mfumko wa bei ni mkubwa sanasana Alisema Dkt Samia.


Hata hivyo ameeleza kuwa Kuendana na mfumko huo wa bei Nchi mbalimbali zinachukua hatua za kurekebisha ili wananchi wasiumie katika mfumko huo wa bei ikiwemo  Tanzania.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI